Kwanini kabila la Dani limeondolewa kwenye Ufunuo 7?

Kwanini kabila la Dani limeondolewa kwenye Ufunuo 7?

SWALI: Hujambo ndugu.Nina ulizo kuhusu kabila 12 ya Yakobo (Israeli) katika mwanzo 49 tunaona kabila la DANI lipo, lakini katika ufunuo 7 kabila la Dani halipo badala yake lipo manase. Kwanini?


JIBU: Katika kitabu cha Ufunuo sura ya 7, kabila la Dani halionekani miongoni wa watu wale watakaoitiwa muhuri siku ya mwisho ili kuiamini Injili itakayokuja kuhubiriwa pale Israeli..Sasa Mungu hakulisahau kabila hilo, hapana bali aliliondoa kwa makusudi kabisa pale na kuliweka hilo la manasae.

Lakini ni kwanini Mungu afanye vile?.. Tukijua jambo hilo jinsi laana za Mungu zilizo kali basi na sisi hatutauchezea wokovu wetu tuliopewa sasa na Mungu wetu.. Kwasababu neema ikishaondoka imeondoka kweli kweli.

Sasa tukisoma kwenye biblia Mungu alishatoa angalizo hili tangu zamani…

Kutoka 20:2 “Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.

3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”

Unaona Mungu alisema kabisa katika amri zake, kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu, na pia anapatiliza maovu yao hata kizazi cha tatu na cha nne..ikiwa na maana kuwa ukifanya dhambi ya makusudi baada ya kuujua ukweli mapatilizo yake yanaweza kuendelea hata kwa vizazi vya wanao huko mbele.

Na tena alisema katika kitabu cha Mambo ya walawi..

Walawi 18:27 “(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)

28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.

29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, NAFSI HIZO ZITAKAZOYAFANYA ZITAKATILIWA MBALI NA WATU WAO”.

Sasa kabila la DANI lilikuwa ni kabila mojawapo la makabila ya Israeli, na kwamba kabila hili lingetakiwa lionyeshe kielelezo kwa watu wa Mataifa kuwa Mungu wa Israeli ndio Mungu na ndiye pekee anayepaswa kuabudiwa,..Lakini lilifika wakati hilo kabila lenyewe likaamua kumuacha Mungu na kwenda kusimamisha SANAMU katika mji wake, na kuiabudu na kuitolea kafara..Ni kabila pekee katika biblia nzima liliokuwa na ujasiri wa kufanya jambo kama hilo..Habari yote hiyo unaweza kuisoma mwenyewe katika kitabu cha Waamuzi sura ya 17 na 18

Sasa jambo hilo lilimfanya Mungu, alifute katika mpango wake wa wokovu..(sawasawa na Neno lake alilolisema) na ndio maana hapo tunaona katika kitabu cha ufunuo ambacho kinazungumzia habari za siku za mwisho, wakati ambapo wana wa Israeli watarejeshewa tena neema hii ya wokovu tuliyonayo sisi, kabila hilo la Dani halitakuwepo katika hesabu hiyo.

Hiyo inatukumbusha na sisi, tusipoizingatia neema hii ya wokovu, tukawa tunaifanyia mzaha, tunajiweka hatarini kwa Mungu kutuacha na kwenda kwa wengine.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Kwanini kabila la Dani na Efraimu hayaonekani yakiorodheshwa miongoni mwa yale makabila 12 ya Israeli katika Ufunuo 7?

MISTARI SHETANI ANAYOITUMIA KUWAANGUSHA WATU

KITABU CHA UZIMA

JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

MIHURI SABA

MISTARI SHETANI ANAYOITUMIA KUWAANGUSHA WATU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments