Biblia ina sura ngapi?

by Admin | 19 December 2022 08:46 pm12

Biblia ina Aya ngapi?

Jibu: “Aya, Sura, na Mlango” ni Neno moja. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66, na kila kitabu kina Aya zake (au sura zake), na kila Aya ina mistari yake.

Kwamfano kitabu cha kwanza cha Mwanzo kina Aya/Sura hamsini (50), na kila Aya/ Sura ina mistari yake.. Kwamfano Aya ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo ina mistari 31.

Kwahiyo tukiuliza biblia ina Aya/Sura ngapi, jibu lake ni kuwa ina Aya nyingi kufuatana na Vitabu vyake. Jumla ya Aya/sura zilizopo katika vitabu vya Agano la kale ni Aya 929, na Aya zilizopo katika vitabu vya Agano jipya ni Aya 260, Hivyo jumla ya Aya zote za vitabu vyote vya biblia ni Aya 1,189.

Je unafahamu kuwa huwezi kuielewa biblia kama hujapokea Roho Mtakatifu?.. Ili uielewe biblia ni lazima umpate Roho Mtakatifu na kanuni ya kumpokea Roho Mtakatifu ni kumwamini Yesu Kristo kwanza kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kisha kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha kabisa, na baada ya hapo kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo na hapo Roho Mtakatifu atakuja juu yako.

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40  Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

Kuna Mbingu ngapi?

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Nini maana ya tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu?

Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/12/19/biblia-ina-sura-ngapi/