Kuna Mbingu ngapi?

Kuna Mbingu ngapi?

Je kuna mbingu ngapi? Mbingu saba ni nini?..na kama zipo 7 je mbingu ya kwanza ni ipi, mbingu ya pili ni ipi, mbingu tatu pia ni ipi? na hatimaye zote saba?..

JIBU:  Katika biblia tunasoma kumetajwa uwepo wa mbingu tatu tu.

2Wakorintho 12:2 ‘Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu’.

Huyu ni Paulo aliyenyakuliwa mpaka mbingu ya tatu. Sasa biblia haijataja uwepo wa mbingu nyingine zaidi ya hizi tatu. Na pia haijazitaja mbingu hizo tatu ni zipi..Lakini kwa Neema za Bwana na kwa kuyachunguza maandiko tunaweza kuzijua ni zipi.

Ipo mitazamo kadhaa juu ya hizi mbingu tatu zilizotajwa hapo juu…Lakini inayojulikana na wengi ni kwamba Mbingu ya kwanza ni hili anga tulionalo ambalo lina hewa yetu ya oksijeni tunayoivuta, kadhalika lenye mawingu na ambalo linanyunyiza mvua..

Na mbingu ya pili ni ile ya juu zaidi yenye magimba ya vimondo, nyota na sayari

Na mbingu ya tatu ni ile ambayo Malaika watakatifu wapo.

Huu ndio mtazamo unaojulikana na wengi. Lakini upo pia mwingine ambao ndio tunaamini ni wa ukweli na huo ni kama ufuatao.

1. Mbingu ya Kwanza: inahusisha anga lote tunaloliona kwa macho…yaani sayari, nyota, jua, mwezi, mawingu, vimondo n.k

2.Mbingu ya Pili: Ni mbingu isiyoonekana kwa macho ijulikanayo kama PARADISO au PEPONI. Ni mahali ambapo roho za watakatifu waliokufa katika Imani ya Yesu Kristo zinahifadhiwa. Mtakatifu anapokufa mwili wake unakwenda kuzikwa kaburini, unaoza lakini roho yake inachukuliwa na malaika watakatifu na kupelekwa paradiso au peponi mahali ambapo pana raha na pumziko, ambapo atakutana na roho nyingine za watakatifu waliokufa katika Imani.

Kwa pamoja watakaa huko paradiso wakingojea siku ya unyakuo ifike ambapo, siku hiyo itakapofika watarudi kuichukua miili yao ya asili na kisha kufumba na kufumbua watabadilishwa pamoja na wale watakatifu walio hai na kwa pamoja watapaa kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni kwenda kuingia katika mbingu ya Tatu.

Yule mhalifu aliyesulubiwa na Bwana Yesu pale msalabani alipelekwa mahali huko ambako Bwana Yesu alimwambia atakuwa naye. (peponi).

3.Mbingu ya Tatu: Ni mahali ambapo Bwana Yesu Kristo yupo pamoja na malaika watakatifu, huko ndiko Bwana alikosema amekwenda kutuandalia makao. Huko hawaingii watu wasio kuwa na miili ya utukufu. Ni sehemu ya raha isiyo na kifani…Mambo yaliyomo humo biblia inasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, mambo ambayo Mungu kawaandalia wale wamchao.(1Wakorintho 2:9).

Hivyo jibu jepesi ya kwamba kuna mbingu ngapi kibiblia? Jibu ni tatu tu kama tulivyoziona hapo juu. Na wala hakuna mbingu saba.

Hivyo tujitahidi tuingie katika mbingu hiyo ya tatu kwa kuuvua utu wa kale wa dhambi na kuvaa utu mpya.

Waefeso 4:22 “mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;

23 na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;

24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

25 Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake”

Na pia biblia inasema katika..

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”

Bwana akubariki.

Tafadhali share na wengine. Maran atha


Mada Nyinginezo:

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

Je! Mbinguni Kutakuwa na kula na kunywa?.

Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?

MBINGUNI YUPO NANI SASA?

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

MBINGUNI NI WAPI?

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
JULIUS CHACHA
JULIUS CHACHA
1 year ago

Haya masomo naweza kuyapata kwa njia ya Whatsapp?

Richard Ngazi
3 months ago
Reply to  Admin

Baadaye