Swali: Biblia inasema tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, maana yake nini?
Jibu: Tusome.
Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.
Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.
Mfano wa Mungu, ni UTU WA NDANI, yaani vitu vyote vinavyopatikana ndani ya roho na nafsi ya mwanadamu, kama vile Furaha,upendo, amani, hasira, wivu, ghadhabu, huruma n.k. Huo ndio mfano wa Mungu, ndio maana utaona kama Mungu alivyo na hasira, mwanadamu naye ana hasira, kama Mungu alivyo na wivu, mwanadamu naye ana wivu, kama Mungu anavyotawala, mwanadamu naye anatawala n.k.. Hiyo yote ni kwasababu kaumbwa kwa mfano wa Mungu. Ndio maana biblia pia inawataja wateule wa Mungu kama miungu.
Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?. Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka)”.
Lakini sura ya Mungu ni utu wa nje… yaani mwonekano wa nje kama macho, pua, mdomo, mikono, miguu, masikio n.k. Kwaufupi umbile la miili yetu ni nakala ya umbile la Mungu. Hii miili haikubuniwa tu, na tukapewa sisi, hapana!. Bali Mungu aliinakili kutoka katika umbo lake mwenyewe na mwonekano wake.
Na hilo umbo akalitengeneza kwa malighafi ya nyama, ndio likawa sisi… Lakini la kwake limetengenezwa kwa malighafi gani? Hakuna anayejua, lakini linafanana kimwonekano na miili yetu.
Ni sawa na ile midoli ya plastiki, inayoning’inizwa masokoni, ile imetengenezwa kwa sura ya mwanadamu…mwili wa mdoli ule ni malighafi yake ni plastiki na wa mwanadamu ni wa nyama, lakini kimwonekano inafanana, ingawa mwanadamu si mdoli.. Kadhalika na sisi tunafanana na Mungu kimwonekano, lakini malighafi iliyounda umbo lake hilo la kiroho, hakuna anayejua.
Kwahiyo sisi tumeumbwa kwa mfano kamili wa Mungu, Ndio maana sehemu nyingi Mungu anahubiri tufanane na yeye katika utu wetu wa ndani…kwasababu inawezekana kabisa sisi kufanana na yeye kwamaana katuumba kwa mfano wake. Kama yeye ni mwenye upendo, na sisi anataka tuwe na upendo wakati wote kama yeye, kwasababu, katuumba kwa mfano wake. Hawezi kututwika mzigo mzito ambao anajua hatutaweza kuubeba.. Kwahiyo alivyotuambia kwamba tuwe na upendo, na wakamilifu, anajua kabisa jambo hilo linawezekana kwetu, kwasababu sisi ni kama yeye..
Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”
Wanyama hawajaumbwa kwa mfano wa Mungu ndio maana hawajaamriwa tuliyoamriwa sisi, kwasababu pengine yangekuwa ni juu ya uwezo wao,. Lakini sisi, mema yote yapo chini ya uwezo wetu endapo tukiamua… “Kuwa wakamilifu duniani na kufanana na Mungu inawezekana kwa asilimia zote”.(Zaburi 16:3).
Na hatuamui kwa midomo tu bali kwa vitendo, pale tunapotubu na kumpokea Roho Mtakatifu, hapo unashuka uwezo juu yetu wa kutugeuza kuwa kama Mungu,.. Ulikuwa unamchukia ndugu yako, sasa hiyo chuki inahama, badala ya kumchukia ndugu yako unakuwa unachukia dhambi, hivyo unakuwa kama Mungu. N.k
Bwana azidi kutubariki sote.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya ‘Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu’ ?
Nguo za magunia katika biblia ni zipi?
Kikuku/vikuku ni nini katika biblia?
Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)
THAWABU ZA SIRI, ZA WATAKATIFU MBINGUNI.
Rudi nyumbani
Print this post
Amina somo zuri sana utukufu kwa Mungu kwa ufafanuzi mzuri wana wa Mungu.🙏🤝👏👏
Amen uzidi kubarikiwa..
Amina, Maanake Mungu akinitazama mimi anamwona kristo ikiwa natenda mapenzi yake na kuwa mtakatifu kweli..
Amen