Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.

by Admin | 28 May 2023 08:46 pm05

Swali: Katika 1Nyakati 21:5 tunasona waliohesabiwa kwa Israeli na Yuda jumla ni  askari 1,570,000 lakini tukirudi  katika 2Samweli 24:9 tunaona jumla ya  idadi ya askari waliohesabiwa walikuwa ni 1,300,000 kwa Yuda na Israeli, je biblia inajichanganya?.

Jibu: Turejee,

1Nyakati 21:5 “Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga”.

Tusome tena…

2Samweli 24:8 “Nao walipokwisha kuzunguka nchi yote, wakaja Yerusalemu mwisho wa miezi kenda na siku ishirini. 

9 Naye Yoabu akamtolea mfalme jumla ya hesabu ya watu; nao walikuwa wa Israeli mashujaa wenye kufuta panga mia nane elfu; nao wa Yuda walikuwa watu mia tano elfu”.

Ni kweli katika mistari hii miwili, panaonyesha tofauti ya Askari waliohesabiwa, tunaona kitabu kimoja kinataja idadi ya juu sana, na kingine kinataja idadi ya chini, sasa swali ni je biblia inajichanganya?

Jibu ni la! Biblia haijichanganyi kwasababu ni kitabu kilichovuviwa na Roho Mtakatifu. Fahamu zetu zinaweza kujichanganya katika kuielewa biblia  lakini kamwe biblia haijawahi kujichanganya, hususani panapotokea habari moja kunukuliwa na waandishi wawili tofauti, kwasababu kama biblia itakuwa na makosa sehemu yoyote, basi kitabu kizima kitakuwa na mapungufu na hivyo hakiwezi kuwa kitabu kitakatifu.

Lakini mpaka Roho Mtakatifu aruhusu kidumu kwa nyakati zote na vizazi vyote ni wazi kuwa biblia yenye vitabu 66 ni maandishi matakatifu na ya kuaminiwa asilimia 100, kwaajili ya maarifa sahihi ya kiMungu, na haina makosa yoyote.

Sasa tukirudi katika hiyo habari tunayoisoma katika vitabu hivyo viwili (1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9) kila mwandishi alijaribu kunukuu aina ya askari waliohesabiwa..

Mwandishi wa kwanza wa kitabu cha 2Samweli 24:9 alinukuu idadi ya Askari ambao walikuwa ni MASHUJAA TU! Ambao idadi yao ilikuwa ni hiyo 1,300,000 Na Mwandishi wa pili wa kitabu cha 1Nyakati 21:5 alinukuu idadi ya Askari wote kwa ujumla (Waliokuwa mashujaa na wasio mashujaa)..ndio maana utaona idadi imeongezeka mpaka kufikia hiyo 1,570,000. Kwahiyo biblia haijichanganyi.

Ilikuwepo tofauti ya Askari wa kawaida na waliokuwa Mashujaa, waliokuwa mashujaa na wale waliokuwa wakongwe na wazoefu katika vita wenye uwezo mkubwa wa kupambana, kwamfano utaona Mfalme Uzia biblia inaonyesha alikuwa na Askari wa kawaida na waliokuwa mashujaa, waliozoea vita, wepesi na hodari wa vita.

2Nyakati 26:11 “Zaidi ya hayo Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, sawasawa na hesabu walivyohesabiwa na Yeieli mwandishi, na Maaseya msimamizi, chini ya mkono wa Hanania, mmojawapo wa maakida wa mfalme. 

12 Hesabu yote ya wakuu wa nyumba za mababa, WATU MASHUJAA, ILIKUWA ELFU MBILI NA MIA SITA.

13 Na chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la askari, mia tatu na saba elfu, na mia tano, ambao walipigana vita kwa nguvu nyingi, kumsaidia mfalme juu ya adui”.

Je unaliamini Neno la Mungu?

Je unajua Bwana Yesu alisema kuwa ”Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni (Mathayo 7:19 )??”

Je ni matunda gani unayozaa?..Mazuri au mabaya..

Mathayo 7:17 “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18  Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

19  Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni”

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?

USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA!

KUNA NGUVU YA ZIADA KATIKA KULING’ANG’ANIA KUSUDI LA MUNGU.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/05/28/swali-je-idadi-ya-askari-waliohesabiwa-katika-1nyakati-215-na-2samweli-249-inajichanganya/