Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;

by Admin | 27 June 2023 08:46 am06

SWALI: Nini maana ya mstari huu Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana”


JIBU: Rafiki anayezungumziwa hapo ni rafiki wa kweli ambaye humwazia mema mwenzake, Hivyo inapotokea umeumizwa kwa maneno ya Ukweli aliyokuambia, ni bora kuliko kusifiwa na watu ambao nyuma yake ni maadui zako.

Ukweli unaomiza, ni kimelea cha upendo sahihi wa ki-Mungu. Bwana Yesu alikuwa ni mtu anayewaeleza ukweli watu wote, hususani wale mafarisayo kwa mambo ya kinafiki waliyokuwa wanayafanya kinyume na Neno la Mungu,(Mathayo 23) jambo ambalo makutano walishindwa kufanya kinyume chake walikuwa wanawasifia tu masokoni kila walipowaona, lakini matokeo yake ikawa ni wao kumchukia  Yesu badala ya kumpenda.

Mtume Paulo alilikemea kanisa la Galatia, kwa tabia yao ya kurudia mafundisho manyonge kiwepesi, ambayo walikuwa wameshayaacha huko nyuma mpaka akawakemea na kusema hamna akili, ni nani aliyewaloga?. Wao walitegemea kuambiwa mambo ya faraja wakati wote, lakini haikuwa hivyo wakati huu, bali lilikemewa sana na Paulo, na ndio maana akasema maneno haya;

Wagalatia 4:16  Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?

Lakini alikuwepo Yuda ambaye alimsaliti Bwana wake kwa kumbusu, akijifanya kama anampenda kumbe, anamundia njia ya kumsaliti.

Maana yake ni kuwa, ukikaa na ndugu, ambaye anakueleza ukweli unaokupasa hata kama ni kwa kukumea au kukurapia, na unakuumiza mpende huyo kuliko makundi ya watu wanaokusifia wakati wote hata pale unapokosea. Ukikaa katika fundisho ambalo unakemewa dhambi na mambo yako mabaya na mwenendo usiostahili, ni heri hapo kuliko kubaki katika mafundisho ambayo yanakusifia na kukufariji wakati wote.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?

VITA DHIDI YA MAADUI

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

USIWE ADUI WA BWANA

Haini ni mtu gani? Mithali 13:2

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/06/27/jeraha-utiwazo-na-rafiki-ni-amini/