je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?

by Admin | 5 October 2023 08:46 am10

SWALI: Maandiko yanasema tusilaani, je! Paulo aliwalaani wagalatia na wakorintho?

Wagalatia 1:8  Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9  Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

1Wakorintho 16:22  Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.

Mtume Paulo alipokwenda katika Galatia na kuwakuta baadhi ya watakatifu wa pale wamegeukia injili nyingine, iliyoletwa na wayahudi, inayosema  ili mtu ahesabiwe haki ni lazima amwamini Kristo pamoja na sheria ya Musa, zaidi ya vile mtume alivyofundisha kwamba kinachoweza kumwokoa mtu ni Imani tu katika Kristo!. Sasa alipoona wamefikia hatua hiyo mbaya ndipo aliposukumwa kusema  maneno hayo makali  kwa wagalatia , kwamba  “mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo waliyoipokea kwake, na alaaniwe”.

Lakini ni vema kufahamu kuwa kauli hii na ile ya 1Wakorintho 16:22 imetumiwa vibaya na baadhi ya wakristo kwa vizazi vingi, kwamba kwa ajili ya injili tunaruhusiwa kuweka laana kwa watu.  Lakini je! Paulo aliwaalaani watu wale?

Jibu la! Kwasababu kama angekuwa ameruhusiwa kuwalaani maadui na wanaokwenda kinyume na , yeye basi asingesema tena maneno haya ya kubariki katika Warumi 12:14

Warumi 12:14  Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

Na isitoshe mtume Paulo alikuwa anawaombea sana rehema ndugu zake  Wayahudi waliopotoka, mbali na neema (Warumi 10:1)

Kama hakuwalaana Je! Katika vifungu hivyo alimaanisha nini?

Hilo Neno kulaani, tukisoma katika tafsiri ya awali ya biblia ya kigiriki  linasomeka kama “Anathema”

Ambalo linamaanisha “mtu aliye chini ya laana/Hukumu ya Mungu”

Hivyo katika vifungu hivyo, Mtume Paulo aliposema “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe” Alimaanisha Hivi;

Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na awe kama mtu aliye chini ya laana ya Mungu”

Na ndio maana mtume Paulo katika hiyo nyaraka yake mbeleni alieleza kwa mapana zaidi, jinsi gani watu waliokuwa wanategemea sheria ili kuwaokoa walivyokuwa chini ya laana ya hukumu. Soma;

Wagalatia 3:10  Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

Kwa hitimisho ni kuwa, mtume Paulo hakuwalaani wakorintho au wagalatia. Bali aliwaeleza uhalisi, madhara ya kuipotosha injili ya Kristo. sisi kama wakristo hatupaswi kuwalaani watu ambao wanatupinga/ au wanahubiri injili inayopotosha, bali ni kuwaombea rehema, wageuzwe, lakini bila kuwaficha matokea ya kutenda kwao huko, Kwamba wapo chini ya laana ya Mungu na hivyo waogope! Kwasababu hukumu ipo.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?

MWAGA DAMU YAKO KWA AJILI YA BWANA.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/10/05/je-paulo-aliwalaani-wagalatia-na-wakorintho/