Jibu: Tusome.
Marko 6.7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; 8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni; 9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. 10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale”
Marko 6.7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;
9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili.
10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale”
Hapo Bwana aliwakataza wasichukue chochote katika safari yao, maana yake huko wanakokwenda watavipata vyote, wasitie wasiwasi, kwamaana endapo wakianza kutia wasiwasi na kuvisumbukia vitu hivyo kwamba huko wanakokwenda watakula nini, watalala wapi, watavaa nini..itawasababisha kupoteza umakini wa hiyo kazi wanayoiendea, itawagharimu kuanza kwanza kutafuta fedha za kutosha, itakayowawezesha kwenda kukaa siku hizo zote na kurudi.. Hivyo Bwana kwa kulijua hilo akawaambia wasibebe chochote hata chakula kwasababu Mungu atawapatia huko waendako.
Lakini pamoja na kwamba aliwaambia wasibebe chochote, mwisho aliwaambia “isipokuwa fimbo tu”
Sasa kwanini fimbo?
Fimbo si chakula, wala si fedha..bali ni kifaa ambacho kilikuwa kinawasaidia watu katika kutembea.. Kwa nyakati zetu hizi, mara nyingi ni wazee ndio wanaotumia fimbo, lakini zamani marika yote walikuwa wanatembea na fimbo, kwasababu kuna nyakati za kutembea umbali mrefu, na kupanda milima na kushuka, hivyo fimbo ilikuwa ni kifaa cha msaada sana, katika hayo mazingira..hususani katika kupandia milima.
Hivyo wanafunzi katika kwenda kuhubiri kwao, hapana shaka watapanda milima mingi na mabonde mengi ili kuwafikia kondoo wa Mungu waliotapakaa huko na kule, hivyo kifaa hicho ni cha muhimu kwao, ndio maana Bwana akawaambia wakibebe.
Hata sasa, agizo la Bwana ni hilo hilo, popote tuendapo, atuagizapo kwenda kuhubiri, tusiangalie hali tulizonazo…kwasababu huko tuendapo atatufungulia mlango wa kupata riziki, sisi tufikiri tu kusudi lake, mengine tumuachie yeye..Ndio maana baadaye tunaona wanafunzi waliporudi walitoa ushuhuda kuwa hawakupungukiwa..
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? WAKASEMA, LA!”
Bwana ni Yule Yule, hajabadilika kama aliwatuma wanafunzi wake bila chochote lakini hawakupungukiwa katika safari zao, hata sisi atakapotutuma hatutapungukiwa. Tunachopaswa kufanya ni kumwamini tu na kujinyenyekeza chini yake na kuukubali utumishi wake kwa moyo wote. Hayo mengine tumwachie yeye, atahakikisha anatuhudumia.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)
KUNA WAKATI YESU ATAPITA NA WATU HAWATAJUA.
Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?
TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.
Rudi nyumbani
Print this post