Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?

Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?

SWALI: Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi?

Kwanini kuna mahali Bwana Yesu anawaita wale aliowaita mitume, na sehemu nyingine anawaita wanafunzi, tofauti yao ni ipi? Au ni kitu kimoja?


JIBU: Si kila mwanafunzi ni mtume, lakini kila mtume ni lazima awe mwanafunzi wa Yesu.

Mwanafunzi ni mtu ambaye anaketi chini kufundishwa, kupewa ujuzi au utashi au maarifa ya kumsaidia kuishi au kufanya jambo Fulani, Na Bwana Yesu naye alikuwa na watu wa namna hiyo hiyo,

Lakini kumbuka si wote waliomfuata waliitwa wanafunzi wake, isipokuwa wale tu waliokidhi vigezo vyake alivyoviweka, na vigezo vyenyewe ndio hivi;

Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,

26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.”.

Lakini Mtume maana yake ni “aliyetumwa”,   Wale walioitwa na Bwana Yesu na kuandaliwa kwa jukumu Fulani maalumu waliitwa mitume, ambao walikuwa kumi na mbili tu kwa wakati ule. Na kusudi lenyewe waliloitiwa lilikuwa hili;

Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa Dahari”.

Mitume pia waliendelea kuitwa na Kristo hata baada ya yeye kuondoka duniani.. Mfano utawaona  mitume  kama  Paulo,  Barnaba, na Epafrodito (Wafilipi 2:25)

Hata kwa wakati huu wa sasa, watumishi wote wa Mungu wanaofanya kazi kama waliyoifanya mitume, Yesu anawatambua kama mitume wake, hawa ni Zaidi ya wanafunzi, kwasababu hawawi wakristo tu peke yake, bali Zaidi wanajitaabisha kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

KUNA WAKATI YESU ATAPITA NA WATU HAWATAJUA.

JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.

Nini maana ya “Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii”?

USITAFUTE KUKANWA NA BWANA SIKU ILE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments