JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.

JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.

Kuna maneno haya ambayo mtume Paulo alisema..

Wagalatia 1:15 “Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,

16 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;

17 WALA SIKUPANDA KWENDA YERUSALEMU KWA HAO WALIOKUWA MITUME KABLA YANGU; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski”.

Tukisoma maneno hayo tunaweza kuona kuwa kipindi kile kulikuwa na utamaduni Fulani, kwamba ikitokea mtu ana wito wa kumtumikia Mungu, ni lazima kwanza, apande kwenda Yerusalemu (kanisa lilipoanzia), akaonane kwanza na wale mitume wa Bwana ambao ni nguzo, kama vile Petro, na Yohana, ili atambuliwe au awekwe kwanza chini ya mafundisho yao ndipo akatumike,Tukisoma maneno hayo tunaweza kuona kuwa kipindi kile kulikuwa na utamaduni Fulani, kwamba ikitokea mtu ana wito wa kumtumikia Mungu, ni lazima kwanza, apande kwenda Yerusalemu (kanisa lilipoanzia), akaonane kwanza na wale mitume wa Bwana ambao ni nguzo, kama vile Petro, na Yohana, ili atambuliwe au awekwe kwanza chini ya mafundisho yao ndipo akatumike,

Lakini tunamwona mtu kama Paulo alikuwa wa tofauti sana, yeye baada ya kuamini, hakujisumbua kwenda kutafuta kukaa chini ya watu hao wakubwa wenye vyeo, bali, aliondoka na kwenda zake mbali mahali panapoitwa Arabuni, kwa muda wa miaka mitatu huko akiutafuta uso wa Mungu.

Na hata aliporudi, biblia inatuambia hakusubiri kwanza akatambulike kwenye makanisa ya wakristo ndipo akahubiri injili, bali, alianza kuhubiri injili hivyo hivyo, wao walichosikia tu ni kwamba yule aliyeliharibu kanisa zamani sasa hivi anamuhubiri Kristo. Sio kwamba alikuwa anajionyesha yeye anajua Zaidi hapana, bali hakuona umuhimu wa kufanya hivyo, kana kwamba ni kitu cha lazima sana.

Wagaliatia 1:21 “Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia.

22 Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo;

23 ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani.

24 Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu”.

Pengine walipomuona anafanya kazi kwa bidii wengine walianza kuulizana je, mnamtambua huyu kwenye makanisa yenu? Wengine wakasema hapana, hatumjui Je! Mitume kule Yerusalemu wanamtambua? Wanasema hapana hawamtambui? Sasa katokea wapi huyu na injili hii ya moto namna hii?

Lakini hilo halikumfanya Paulo asihubiri injili, kisa hatambuliwi na mitume ambao ndio nguzo, bali aliitenda kazi akimwangalia yeye aliyemwita yaani YESU KRISTO. Na baada ya miaka mingi sasa, kama 14 hivi ndipo tunamwona anapanda kwenda Yerusalemu kuonana na mitume, kusikiliza mausia kutoka kwao. Lakini anasema alipofika kule hawakumuongezea chochote badala yake alimkuta Mtume Petro amekwenda kinyume na Imani, na hivyo akamkemea mbele ya wote.

Wagalatia 2:6 Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu;…….

11 Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu.

12 Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.

13 Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao.

14 Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?

Mpaka mwishoni kabisa mwa huduma yake, Paulo anashuhudia kwa uvuvio wa Roho kuwa yeye ndiye aliyefanya kazi kuliko hata mitume wengine wote waliomtangulia. Na sisi tunalithibitisha hilo.

Sasa habari hiyo inatufundisha nini sisi wa kanisa la leo.

Kumbuka wenye vyeo na wenye sifa waliojulikana zamani ni 12 tu, ndio wale mitume wa Bwana Yesu, lakini leo hii wenye vyeo na wenye sifa katikati ya kanisa la Mungu, idadi yake haihesabiki. Kiasi kwamba watu wengi wameshindwa kumtumikia Mungu, kisa tu, kuna ngazi zimewekwa hapo juu yao, ambazo ni lazima wazipitie kutoka kwa viongozi wao waliowatangulia au wapate kibali kwanza cha kufanya hivyo.

Ndugu sio lazima upokee kila agizo chini ya kasisi wako, ndio ni vizuri kufanya hivyo, ikiwa huwekewi vikwazo, au hutumii nguvu nyingi kutumika, lakini mara nyingi zinakwamisha huduma za watu wengi sana Mungu alizoweka ndani ya mioyo yao. Wakati mwingine utaambiwa pitia shule ya biblia miaka 4, ndipo uhitimu utumike.

Si kila kitu ni cha kutafuta kujiweka chini ya mtu Fulani kwanza, wakati mwingine Mungu anataka aanze kutembea  wewe peke yako, akufundishe wewe kama wewe. Maadamu nia yako ni njema kwake, na una lengo kweli la kuujenga ufalme wa Mungu hilo tu linatosha.  Kumbuka hiyo haimaanishi kuwa usijifunze kutoka kwa wengine hapana, lakini ujijengee akilini kuwa, Mungu amekuita umtumikie yeye, na si wanadamu.

Alilolichagua mtume Paulo, ndio hilo na likamsaidia sana,. Nasi pia tujitahidi kupunguza mizigo ya kuwategemea wanadamu, zama hizi ambazo watu wa namna hiyo wapo wengi, unaweza ukajikuta unadumaza huduma Mungu aliyoiweka ndani yako.. Wewe fanya utakuja kuwafuata baadaye.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

JINSI PAULO ALIVYOPAMBANA NA UJINGA WA ROHONI.

Makao ambayo Yesu alikwenda kutuandalia ni yapi?

Nini maana ya “Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii”?

Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?

ANGALIENI MWITO WENU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments