by Admin | 18 January 2024 08:46 am01
Swali: Kuvuta Makasia maana yake nini?
Likiwa moja linatiwa ”Kasia”, yakiwa mengi ni “Makasia” … Hizi ni “Zana” ya kukisaidia chombo kutembea juu ya maji. Zana hii kwa mwonekano ni kama “Mwiko mkubwa”, (tazama picha juu), ambapo mabaharia walipoyavuta basi chombo kilisogea mbele..
Yona 1:13 “Lakini wale watu WAKAVUTA MAKASIA kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana”.
Unaweza kusoma Zaidi kuhusu makasia katika mistari ifuatayo; Marko 6:48, Yohana 6:19, Isaya 33:21, na Ezekieli 27:6.
Je ni nini tunajifunza katika habari ya Yona na mabaharia hawa kuvuta makasia kurudi pwani?.. Fungua hapa >>>YONA: Mlango 1
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/01/18/makasia-ni-nini-yona-113/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.