JE! MWAMBA HALISI NI NINI KULINGANA NA BIBLIA?

by Admin | 28 January 2024 08:46 pm01

Je! Umejengwa kweli juu yake?

Ukimuuliza mtu, mwamba ni nini, ni rahisi kukujibu YESU. Jibu ambalo ni sahihi, maandiko yanatuthibitishia hilo Yesu kuwa Yesu ni mwamba (Mathayo 21:42, 1Wakorintho 10:4). Lakini lazima ufahamu pia  MWAMBA mwenye anasemaje, kuhusu yeye mwenyewe alivyo.

Ni maneno ambayo tunayasoma lakini si rahisi kuyatafakari kwa ukaribu, embu tusome tena, halafu utaona mwamba alimaanisha nini. (Zingatia vifungu vilivyo katika herufi kubwa) Soma kwa utulivu.

Mathayo 7:24  Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

28  Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29  kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Umeelewa? Vema hayo maneno?

Kumbe mtu  yeyote anayesikia maneno ya Yesu. Hapo hapo huwa anaanza ujezi.

Lakini tofauti inakuja mahali anapokwenda kujengea,. Yule aliyejenga kwenye mchanga tafsiri yake Yesu anasema, anasikia, lakini hayatendei kazi (Hayafanyi), aliyoyasikia. Hivyo hapo Mchanga, ni KUTOTENDA.

Lakini Yule mwingine aliyekwenda kwenye mwamba tafsiri yake ni anasikia lakini pia anatenda. Hivyo MWAMBA, ni kutenda.

Mwamba sio kumjua Yesu ndugu, mwamba sio kusoma sana biblia na kujua mafumbo na siri zote zilizo katika biblia, mwamba sio kujua kujua tafsiri zote za kigiriki na kiebrania kwenye maandiko, mwamba sio kujua kufundisha vema biblia,.. Sio hivyo vyote.

Mwamba ni KULITENDEA KAZI NENO, Unalolisikia kwake. Hilo tu. Sio kumjua Yesu.

Hatari iliyopo leo, miongoni mwa wakristo wengi, ni kwamba tumejengwa juu ya mafundisho mengi. Lakini hatujajengwa juu ya kutendea kazi mafundisho tunayofundishwa. Ndugu fundisho halikusaidii kuyashinda majaribu, au tufani za mwovu, au dhoruba, au pepo, hapo unafanya kazi ya kuchosha tu,kudumu katika kusikia, kusoma, kusikiliza, bado si suluhisho, kusema nimebarikiwa, nimefunguliwa ufahamu, bado hakukufikishi popote, kama HUTALIISHI hilo Neno.

Ukiwa ni wa kufanya bidii kuliishi NENO moja, wewe ni imara sana kuliko Yule mwenye kujiona anaijua biblia yote

Penda Utakatifu, penda usafi wa moyo, penda kupiga hatua rohoni. Penda matendo mema.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

NAYAJUA MATENDO YAKO.

Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/01/28/je-mwamba-halisi-ni-nini-kulingana-na-biblia/