Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?

by Admin | 20 February 2024 08:46 am02

SWALI: Je! ni sahihi kwa mkristo kufanya biashara za kifedha mitandaoni kama vile Forex, na crypto-currency mfano wa bitcons?


JIBU: Ni vema kufahamu biashara za kifedha mitandaoni kama forex ni nini?

Ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni katika soko la dunia. Yaani ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni, sawa tu ile tuliyowahi kuisikia, ijulikanayo kama Bureau de change, ambayo watu wanakwenda kununua/kuuza pesa za kigeni, isipokuwa hii hufanyika mitandaoni, tofauti na bureau ambayo hufanyika kwa makarati ndani ya ofisi Fulani maalumu. Biashara hii ya forex na nyinginezo Mara nyingi hufanywa na taasisi kubwa za kifedha kama mabenki na makampuni, lakini pia hata watu binafsi.

Ni biashara ya bahati nasibu, inayofanana na michezo ya kubahatisha kitabia.. Lakini ni tofauti kabisa kimaudhui.

Biashara  hii ni ya uwekezaji, ambayo imehalalishwa ki-ulimwengu, japokuwa hatusemi kuwa kila biashara iliyohalalishwa na taifa kuwa ni halali kwa mkristo kufanya, hapana mfano zipo pombe zimehalalishwa kitaifa lakini kwa mkristo sio sawa kufanya biashara kama hizo.

Lakini, biashara hii, haihusishi katika kumdhulumu mtu, au kumlaghai mtu kiakili, apoteze kitu Fulani ili wewe ujilimbikizie fedha zake ambazo hazina mzungumko wowote wa kimaendeleo. Mfano wa hizo ni kama vile “Betting na kamari”. Kwa mkristo kushiriki katika biashara hizo za betting na kamari sio sawa. Kwa urefu wa somo lake pitia link hii >>>JE! KUBET NI DHAMBI?

Lakini Forex na nyinginezo zijulikanazo kama biashara za uwekezaji, zinahitajika sana, kwasababu kama zikikosekana, basi mzunguko wa fedha za kigeni, ungekuwa mgumu sana, na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji uchumi, katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia.

Hivyo tukirudi kwa mkristo, je kufanya biashara hii ni dhambi?

Kimsingi ikiwa anafanya kwa lengo la uwekezaji wake, huku akijua pia ni kwa faida ya uchumi, na hamdhulumu au kumlaghai mtu. Hafanyi kosa. Lakini akiwa na fikra za kikamari, kama vile afanyavyo kwenye betting, Kwake itakuwa ni kosa, kwasababu dhamiri yake inamshuhudia, ameigeuza kama kamari moyoni mwake.

Ndio hapo hili andiko linakuja.

Warumi 14:22  Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.

23  Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.

Maana yake ni kuwa ukiwa na mashaka moyoni mwako kuifanya kazi hii, basi ni heri usifanye kabisa, kwasababu mashaka yoyote ni dhambi. Lakini kimsingi biashara hii sio kosa kwa mkristo, ambaye ana maarifa/elimu ya kutosha juu ya biashara za kifedha katika ulimwengu wa sasa.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/02/20/je-ni-halali-kwa-mkristo-kufanya-biashara-ya-forex/