HAJIRI NI KAMA MLIMA SINAI ULIOKO ARABUNI.

by Admin | 2 April 2024 08:46 am04

(Mfululizo wa masomo yahusuyo Uhuru wa Roho na Utumwa wa sheria).

Jina la Bwana YESU, MKUU WA UZIMA libarikiwe. Karibu tujifunze biblia, Neno la MUNGU wetu lililo Taa na Mwanga wa njia yetu (Zab. 119:105).

Biblia inamfananisha HAJIRI, (yule aliyekuwa “kijakazi” wa Sara na Ibrahimu) na YERUSALEMU YA DUNIANI. Na tena inamfananisha “Ishmaeli” aliyekuwa mwana wa Hajiri na “wale wote walio chini ya utumwa wa sheria” waliopo pale katika mji wa YERUSALEMU uliopo Israeli.

Vile vile “Sara” aliye mwungwana (yaani huru) inamfananisha na YERUSALEMU YA MBINGUNI (mji wa kimbinguni) na mtoto wake “Isaka” inamfananisha na “watu wote wa kimbinguni” (yaani walio huru na utumwa wa sheria)..ndivyo maandiko yanavyosema..

Wagalatia 4:22 “Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.

23  Lakini yule wa mjakazi alizaliwa KWA MWILI, yule wa mwungwana KWA AHADI.

24  Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.

25  Maana HAJIRI NI KAMA MLIMA SINAI ULIOKO ARABUNI, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.

26  Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.”

Sasa maelezo marahisi ya maandiko haya ni kwamba Wana wa Israeli walipokea sheria kutoka kwa Musa alipopanda kule mlima Sinai/Horebu..na kuwaletea wana wa Israeli agano la sheria..ambalo watu wote waliokuwa chini ya hilo walikuwa ni “watumwa wa sheria”..na ndio wayahudi.

Sasa Agano hili la sheria wana wa Israeli walilolipokea kutoka Mlima SINAI,  lililowafunga na kuwafanya kuwa watumwa wa hiyo sheria na ndilo linalofananishwa na HAJIRI (aliyekuwa kijakazi wa Sara), kwasababu Hajiri alikuwa ni mtumwa na wala si Huru. Na mtoto wake Ishmaeli pamoja na wengine wote waliofuata (watoto wa Ishmaeli) bado walikuwa ni wana wa mjakazi tu vile vile.

Lakini Sara hakuwa mjakazi, bali alikuwa HURU pamoja na Mtoto wake Isaka, ikifunua agano la pili la UHURU ambalo ndilo la wale watu waliozaliwa kwa roho, ambao sheria imeandikwa ndani ya mioyo yao na si katika mawe, au makaratasi.

Na hawa ni watoto wa Sara kwa namna ya roho na ndio wana wa YERUSALEMU YA MBINGUNI, kwasababu wote wanaoishi kwa kuongozwa na roho ndio watakaoirithi YERUSALEMU MPYA na ndio wenyeji wao upo kule, lakini wanaoishi kwa sheria ambayo asili yake ni mlima Sinai, hao ni wa Yerusalemu ya duniani.

Na kama vile Hajiri alivyofukuzwa pamoja na mwanae, kwasababu si mwana wa ahadi…vile vile wote wanaoataka kuishi kwa sheria watatengwa na Kristo.

Wagalatia 5:4 “Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema”.

Biblia inatufundisha kuwa tunahesabiwa haki kwa Neema, kwa njia ya Imani na si kwa matendo ya sheria.

Warumi 3:9 “Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.

10  Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

11  Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa Imani”.

Sasa kujua kwa undani tofauti ya Matendo ya sheria na Matendo ya Imani fungua hapa >>NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini tofauti ya Mtumwa, Mjakazi na kijakazi?

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?

KATIKA MLIMA WA BWANA ITAPATIKANA.

NI WAPI UTAKUTANA NA MALAIKA WA BWANA?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/04/02/hajiri-ni-kama-mlima-sinai-ulioko-arabuni/