Njia ya Msalaba ni nini, na Je ipo kibiblia?

by Admin | 6 April 2024 08:46 pm04

Swali: Njia ya msalaba ni nini na Ipi historia ya njia ya msalaba?

JIBU..

Njia ya Msalaba ni Desturi iliyoanzishwa na kanisa Katoliki ambapo waumini wanapita katika mitaa ile Bwana YESU aliyosulubiwa, kuanzia alipotoka kwa Pilato mpaka mwili wake ulipowekwa kaburini.

Kulingana na kanisa Katoliki, kuna vituo 14 ambavyo Bwana YESU alipitia, ambapo  kila inapofika Ijumaa kuu (ile ya pasaka) wakatoliki hupita katika vituo hivyo huko YERUSALEMU kuanzia mahali pajulikanapo kama “ngome ya Antonia” mpaka “kanisa la Roma la ufufuo” (karibia na mahali ambapo Kaburi la Bwana YESU lilikuwepo)..matembezi hayo ni ya mita 600.

Na wale wasiokuwepo Israeli basi watapita karibu na picha kumi na nne (14) zilizochorwa katika kuta za makanisa hayo ya Roma na kusema baadhi ya sala.

Vifuatavyo ni vituo hivyo kulingana na kanisa katoliki.

1. Yesu anahukumiwa kuuawa.

2. Yesu anapewa msalaba na maaskari wa kiroma

3. Yesu anaanguka chini kwa mara ya kwanza.

4. Yesu anakutana na mama yake (Mariamu)

5. Simoni Mkirene anashurutishwa kuubeba msalaba wa Yesu.

6. Veronika anapangusa damu katika uso wa Bwana Yesu.

7. Yesu anaanguka kwa mara ya pili.

8. Yesu akutana na wanawake wa Yerusalemu.

9. Yesu anaanguka mara ya tatu

10. Yesu anavuliwa mavazi yake

11. Bwana Yesu anagongomelewa msalabani

12. Yesu anaisalimu roho yake

13. Mwili wa Bwana Yesu unaondolewa msalabani.

14. Mwili wa Bwana Yesu wawekwa kaburini.

Hivyo ndivyo vituo 14, Bwana Yesu alivyovipitia kulingana na kanisa katoliki.

Lakini vituo baadhi hapo hatuvioni katika maandiko, kwamfano kituo cha 3,7 na 9 cha Bwana YESU kuanguka chini mara ya kwanza, na ya pili na ya tatu havipo katika maandiko..

Vile vile kituo cha 6 kinachomtaja Veronika kufuta damu katika uso wa Bwana YESU hakipo katika biblia..na hata kituo cha 4 cha Bwana YESU kukutana na mama yake hakipo katika biblia!.

Hivyo kama habari hizo hazipo katika biblia hatupaswi kuziamini wala kuzishika kwani huenda ni habari za kutungwa! au zimetolewa katika vyanzo visivyo sahihi, ambavyo havijahakikiwa na Roho Mtakatifu.

Kitabu cha biblia chenye vitabu 66, hiyo ndiyo iliyohakikiwa na Roho Mtakatifu lakini vitabu vingine nje na hivyo vya kwenye biblia ni potofu na vina udanganyifu.

Na Zaidi hatujapewa amri ya kuadhimisha vituo vya Bwana YESU alivyopitia, ndio! Tunaweza kutafakari lakini si kufanyia ibada,..sala za namna hiyo ni ibada za sanamu, kwani zinamfanya mtu aanguke katika zile picha au katika ile mitaa huko Yerusalemu, jambo ambalo ni machukizo.

Kufahamu njia ya Msalaba hasa kibiblia ni ipi fungua hapa >>> NJIA YA MSALABA

Shalom..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.

Matuoni ni nini katika biblia?

MSALABA NI ZANA YA UJENZI WA MAISHA YAKO.

UTHAMINI WITO WA PILI WA YESU ZAIDI YA ULE WA KWANZA.

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/04/06/njia-ya-msalaba-ni-nini-na-je-ipo-kibiblia/