Kuhani wa Oni alikuwa nani?

by Admin | 21 May 2024 08:46 pm05

Swali: Huyu Kuhani wa Oni ambaye binti yake aliolewa na Yusufu, tunayemsoma katika Mwanzo 41:45  je alikuwa ni kuhani wa Mungu au wa kuhani wa miungu ya kiMisri?

Jibu: Terejee mistari hiyo…

Mwanzo 41:45 “Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti POTIFERA, KUHANI WA ONI, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri”.

“Oni” lilikuwa ni eneo katika nchi ya Misri, kama vile ilivyo Mwanza, au Lindi nchini Tanzania au Nakuru Kenya.

Mji huu (wa Oni) Ulikuwa ni mji wa miungu ya kiMisri, na nchi ya Misri yote ilikuwa ni nchi inayoabudu miungu mingi,  ikiwemo Bethshemeshi (soma Yeremia 43:13), sanamu za ng’ombe (1Wafalme 12:28) na mingine mingi (soma Yoshua 24:14).

Hivyo huyu kuhani “Potifera” hakuwa kuhani wa Mungu wa mbingu nan chi (YEHOVA), bali alikuwa ni kuhani wa miungu ya kimisri iliyokuwepo hapo “Oni”, na Yusufu alipofika kule alipewa binti yake awe mkewe.

Na Kwanini ulikuwa hivyo?(yaani kwanini Farao amchagulie mke na si Yusufu ajitafutie mwenyewe?)..

Jibu ni kwamba Farao aliona njia pekee ya kumheshimisha Yusufu na kumfanya apate kibali katikati ya waMisri ni kumuunganisha yeye na familia za watu wa kubwa na wenye hadhi wa nchi ya Misri.(wenye hadhi za kiimani), kwasababu naye Yusufu alikuwa mtu wa kiimani.

Hivyo na mtu wa kiimani na kidini aliyekuwa mkubwa huko ni huyo kuhani wa Oni, ndipo akapewa binti yake aliyeitwa Asenathi. Lakini hata baada ya Yusufu kupewa mwanamke huyo bado hakufuata miungu hiyo ya kiMisri, na Farao alilijua hilo, na wala hakumpatia huyo binti kwa lengo la kugeuza Imani ya Yusufu, bali kumheshimisha.

Lakini kwasababu pia ilikuwa ni mpango wa Mungu iwe hivyo (Yusufu aoe mwanamke wa kimataifa) basi hata mke aliyempata alikuwa ni sahihi kwake na wala hakumsumbua Yusufu baada ya hapo (huwenda hata alimtumikia Mungu wa Israeli baada ya hapo), na Zaidi sana tendo la Yusufu kumwoa Asenathi (binti wa kimataifa) limebeba ufunuo mkubwa juu ya Bwana  YESU KRISTO na BIBI-HARUSI WAKE (yaani kanisa).

Kwa urefu marefu juu ya ufunuo wa maisha  ya Yusufu fungua hapa >>>Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Musa aliua lakini bado Mungu alimchangua kuwaongoza wana wa Israeli, je! Mungu anaruhusu mauaji?

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.

Ni lini na wapi Ibrahimu aliiona siku ya Bwana akashangilia?.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/05/21/kuhani-wa-oni-alikuwa-nani/