Je kumwimbia Mungu kwa kucheza ni sahihi kibiblia?

by Admin | 29 June 2024 08:46 am06

Jibu: Kuna mambo makuu mawili ya kuzingatia katika kulitafakari hili.

    1. KWANINI UNACHEZA

    2. NACHEZAJE

Tutazame moja baada ya lingine.


     1. KWANINI UNACHEZA!

Tafakari umempa mtoto kitu anachokipenda, au mwanamichezo kashinda mchezo wake, au mwanafunzi kapata taarifa za kufaulu mitihani yake, huwa ipo furaha ambayo inaweza kumpelekea kuruka ruka kwa shangwe.

Sasa furaha ya namna hiyo inayompelekea kuruka rukwa kwa shangwe haina nia ya Maonyesho, au majivuno, bali ni mwitikio wa jambo jema linaloendelea au lililotokea.

Na kadhalika tunapofanyiwa jambo na MUNGU (Ambaye kwaasili huwa haishi matukio wala miujiza) zipo hisia zinazoambatana na shangwe, ambapo shangwe hiyo inaweza kuambatana na kuimba kwa kuruka ruka kama ndama!.

Raha ya namna hii inayoambatana na kuruka ruka na kucheza cheza tutaipata Zaidi siku ile tutakapomaliza mwendo, na kutangaziwa na BWANA KWAMBA TUMESHINDA!!, NA HIVYO TUNAUINGIA ULE MJI MTAKATIFU, NA KUKAA HUKO MILELE… Hapo baba, au mama hata kama hupendi kucheza utacheza tu!!.

Malaki 4:2 “Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, NA KUCHEZA-CHEZA KAMA NDAMA WA MAZIZINI”.

Sasa ikiwa kuna ahadi ya sisi kucheza cheza huko mbeleni tutakapomaliza maisha haya na kutangaziwa ushindi.. vipi vipindi vidogo vidogo ambavyo Mungu anatupa ushindi hapa duniani?.. kwamba tulikuwa tunaumwa kiwango cha kufa, sasa Bwana katuponya, ndoa zilikuwa zinayumba sasa Bwana kazisimamisha.

Watoto walikuwa wanasumbua sasa Bwana kawatengeneza, Wokovu ulikuwa huna sasa Bwana kakupa… Kwasababu kama hizo wakati mwingine shangwe inaweza kuzidi mpaka kufikia hatua ya kucheza na kuruka ruka kama ndama huku ukimwimbia Bwana. (Hapo inakuwa ni wewe na Bwana na si wewe na mtu).

Unapozitafakari hizo sababu na nyingine nyingi, hauhitaji au husubiri uambiwe umshangilie Mungu, bali hiyo hali itatoka tu yenyewe ndani yako, na wala haitakuwa na lengo la kutazamwa na watu.

      2. UNACHEZAJE

Hili ni jambo la pili la kuzingatia.. UNACHEZAJE!!.. Ukiona unatafuta mtindo/style ya kucheza wakati wa Sifa, hapo kuna jambo la kutafakari!!!.. Sifa zinazozalika kwa kutafakari matendo makuu ya Mungu, hazinaga step, hazinaga kanuni maalumu, na pia zina staha!!..

Huwezi kumshangilia Bwana kwa staili za disko,..huwezi kutikisa makalio kama wafanyavyo wanenguaje wa disko..huwezi kucheza kwaito, na kushikana shikana na mwingine kama watu wa duniani wafanyavyo.. wengine wapo nusu uchi halafu wanasema wanacheza!..hiyo ni hatari sana.

Sifa za namna hiyo sio kutoka katika roho, bali na za NIA ya mwilini,..ambazo lengo lake kuu ni kutazamwa  na watu na kusifiwa nao au kuwapendeza..na ndizo ambazo mkristo hapaswi kuzifanya.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba iwe katika kuabudu, au kusifu, au kuruka ruka ni lazima yote yafanyike kwa staha na kwa utukufu wa Mungu.

Wafilipi 4:8 “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?

Jicho kucheza ni ishara ya nini?

NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?

Nini maana ya Shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo Ayubu 20:4

HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/06/29/je-kumwimbia-mungu-kwa-kucheza-ni-sahihi-kibiblia/