Jicho kucheza ni ishara ya nini?

Jicho kucheza ni ishara ya nini?

Jicho kucheza cheza maana yake nini?.. au inaashiria nini kiroho?..Je ni ishara ya kwamba kuna mtu ananisema au kuna jambo baya linakwenda kutokea?.


Jibu: Jicho kucheza ni kitendo cha kope ya jicho moja kutikisika.. Hali hii inawatokea watu wengi, katika vipindi tofauti tofauti (Na ni tendo lisilo la hiari).

Katika biblia hakuna mahali popote panaonyesha kuwa jicho kutikisika ni ishara ya jambo Fulani lijalo, wala hakuna mtu aliyewahi kufunuliwa jambo  lolote (lijalo au lililopita) kwa njia hiyo katika biblia…

Isipokuwa kuna vipindi vichache ambavyo hisia za rohoni zinaweza kujidhihirisha katika mwili… Kwamfano mtu anaweza kushukiwa na nguvu za Mungu akahisi mwili wote kutetemeka..mwingine akahisi masikio yanawaka moto, mwingine miguu, mwingine mikono, mwingine jasho mwili mzima n.k Hii inatokea lakini si kwa watu wote, bali kwa wachache… lakini jicho kucheza ni jambo ambalo linawatokea wengi!.

Mwingine akaingia mahali penye mamlaka nyingine mwili ukaishiwa nguvu au akapata msisimko Fulani..Hiyo inaweza kutokea kwa baadhi ya watu ila si wote..L akini katika suala la jicho kucheza si jambo geni, au la watu wachache…bali ni jambo ambalo linawatokea  wengi sana (Zaidi ya asilimi 90 ya watu).

Hivyo si tendo la ajabu kwamba ni ishara ya jambo Fulani lijalo… bali ni misisimko tu ya misuli ya mwili ambayo inaweza kutokea sehemu nyingine yoyote katika mwili, wengine inawatokea katika misuli ya mikono (misuli inaanza kucheza tu yenyewe), wengine katika miguu na sehemu nyingine za mwili. Inapotokea hali kama hii huwa inaisha yenyewe baada ya muda fulani kupita.

Lakini ikiwa kuna kitu ambacho Roho Mtakatifu anataka kukufunulia kupitia hisia za mwili, au kiungo chako…basi kitu hicho kitakuwa Dhahiri kwako atakuambia, lakini pia kumbuka siku zote Roho Mtakatifu hana kanuni moja maalumu ya kusema na mtu kwamba leo akitumia ishara hiyo ya mwili basi kesho atarudia tena kusema na wewe kwa njia hiyo hiyo (inakuwa ni nadra sana).

Maana yake kama leo Bwana kakupa ufunuo kwa ishara ya jicho usitegemee kesho jicho litakapocheza basi ni Bwana anataka kusema na wewe (kamwe usiende katika hayo mazoea)Looking for an affordable yet stylish timepiece? Look no further than our Replica hublot 44mm collection, where luxury meets affordability. These Cheap Diamond Replica Hublot 44mm watches, all under $39, exude elegance and sophistication without breaking the bank. Crafted with precision and attention to detail, our replicas capture the essence of the original Hublot design, making them a perfect choice for those who appreciate quality without the hefty price tag. Experience the allure of a Hublot 44mm watch today and elevate your style effortlessly.. Mahali pekee ambapo unaweza kutafuta kupokea ufunuo mara kwa mara kwa njia hiyo hiyo moja, ni KWENYE BIBLIA.

Kila utakapoishika biblia na kutafuta kuisoma katika utulivu na kumaamisha basi utaisikia sauti ya MUNGU, lakini si kila jicho linapocheza, au mwili unapochemka, au mikono inapowaka moto, au nywele zinaposisimka.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Kijicho ni nini? (Marko 7:22)

Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?

TAA YA MWILI NI JICHO,

Je biblia inatuhubiria kucheza Mieleka au kuitazama? (Mwanzo 32:24)

Je ushabiki wa mpira ni dhambi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments