Nini maana ya’Shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo’Ayubu 20:4

Nini maana ya’Shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo’Ayubu 20:4

Ayubu 20:4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi, 

5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu? 

6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni; 

7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?

Waovu wanayo  ‘shangwe’ maandiko yanasema hivyo,  lakini shangwe yao ni ya muda mfupi tu. Usishangae kuona mtu ni tapeli na muuaji lakini anaishi maisha ya raha, yenye afya, watoto wake wanafanikiwa sana, uso wake unang’aa kila wakati, na biashara zake zinachanua. Ndio! hilo jambo lisikushtushe, kwasababu maandiko hayatuahidi kuwa waovu watapitia shida wakati wote duniani. Hapana.

Tena anasema wataweza kufikia kuwa na ukuu usio wa kawaida mfano wa kuifikia mbingu, ikiwa na maana wanaweza kuonekana hata ni miungu duniani. Lakini hiyo yote ni kwa muda tu, siku watakapokufa habari yao itakuwa imeishia hapo, Biblia inatumia mfano wa ‘Mavi’ jinsi yapoteavyo, ndivyo watakavyopotea watu hao milele.

Hakuna mtu anaweza kukitafuta kinyesi chake alichojisaidia mwaka jana au mwezi uliopita,. Ni wazi kabisa alishakisahau, na tayari kilipofika chooni kiliyeyuka na kuingia katika mfumo wa chemba ya maji machafu, kikatowekea huko. Sasa ndivyo itakavyokuwa kwa mtu Yule ambaye anashindania raha ya dunia hii anaacha kutafuta raha ya kudumu inayotoka kwa Yesu Kristo peke yake.

Zaburi 92:7 Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;

Yesu alisema itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima, kisha upate hasara ya nafsi yako, au utatoa nini badala ya nafsi yako? Ujue kuwa kusudi la wewe kuwepo duniani sio kula na kunywa, au kupanda na kujenga au kuwa milionea au kuwa maarufu. Bali ni kuyatenda mapenzi ya Mungu kwanza kisha hayo mengine yafuate baadaye.

Kubali kubadilika leo Yesu ayaponye maisha yako. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi fungua hapa kwa mwongozo wa kumpokea Yesu maishani mwako >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.

Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?

Beelzebuli ni nani? (Mathayo 12:24).

SHUGHULIKA SANA NA DHAMBI YA KUSAHAU.

Je! tunaweza kuwaamuru Malaika kama tunavyoyaamuru mapepo?

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)

Kumwambia mtu mwenye dhambi kuwa atakwenda kuzimu asipotubu Je! ni kuhukumu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments