(Masomo yahusuyo malaika na uwezo wao)
Swali: Je watu wa Mungu wanaweza kuwaamuru Malaika watende jambo Fulani au watoke na kwenda mahali Fulani kama vile mapepo yanavyoamrishwa kwa jina la Yesu?.
Jibu ni hapana!!. Hatujapewa mamlaka yoyote ya kuwaamrisha Malaika, iwe kwa mapenzi yetu wenyewe au kwa jina la Yesu!. Malaika ni viumbe wanaotii na kufuata maagizo ya Mungu tu! si maagizo yetu, na hakuna mahali popote katika maandiko panapoonyesha au kufundisha wanadamu kuwapa malaika maagizo. Zaidi sana sisi (wanadamu) ndio tuliowekwa chini ya uwezo wa Malaika.
Utaona wakati wana wa Israeli wanatoka Misri, maandiko yanasema Mungu aliwapelekea malaika ambaye aliwaongoza katika njia yao yote, na umati mzima wa Israeli ulionywa na Mungu kumsikiliza Malaika yule kwani Mungu ameweka Neno lake ndani yake, na Zaidi sana Mungu aliwaonya kuwa wasimposikiliza yule malaika hatawasamehe, kinyume chake atawadhuru!.
Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. 21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali”.
Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.
22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.
23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali”.
Kwahiyo elimu ya kuwaamrisha malaika au kuwapa maelekezo haipo kibiblia, huenda uwezo huo tutakuwa nao baada ya kumaliza maisha haya tutakapofika mbinguni lakini kwa wakati huu hatujapewa hayo mamlaka, kwasababu hata Bwana wetu Yesu alipokuwa duniani alijishusha akawa mdogo kuliko Malaika wote..si Zaidi sisi?
Waebrania 2:9 “ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu”.
Sasa kama ni hivyo ni njia zipi tunaweza kuzitumia ili Malaika wafanya yale tunayoyataka sisi.
1.KWA KUMWOMBA BABA
Tukitaka kuona Malaika wanafanya yale tunayoyataka, njia ya kwanza ni sisi kumwomba Baba yetu yetu wa Mbinguni, (tunaomba kwamba atupelekee malaika zake watufanyie hiki au kile) na kama jambo hilo tuliombalo ni mapenzi ya Mungu basi Baba yetu wa mbinguni anawapa amri Malaika wake kutekeleza kile tulichokiomba, au tukitakacho (hapo amri inakuwa imetoka kwa Mungu moja kwa moja na si kwetu). Kama Bwana Yesu alivyomwambia Petro wakati ule alipomkata mtumwa wa kuhani mkuu sikio.
Mathayo 26:51 “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. 52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. 53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, NAYE ATANILETEA SASA HIVI ZAIDI YA MAJESHI KUMI NA MAWILI YA MALAIKA?”.
Mathayo 26:51 “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.
53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, NAYE ATANILETEA SASA HIVI ZAIDI YA MAJESHI KUMI NA MAWILI YA MALAIKA?”.
2. KWA KULITENDA NENO.
Njia ya pili ni kwa kuliishi na kuliltenda Neno la Mungu. Malaika wa Mungu walishapewa maagizo ya kutekeleza yale yote yaliyoagizwa kwenye Neno la Mungu. Kwamfano Neno la Mungu linasema “
Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa Dahari”.
Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa Dahari”.
Sasa mtu anapolitii hili Neno na kutoka kwenda kuhubiria wengine habari njema, hapo bila hata kuomba kwamba Malaika wa Mungu waende na yeye, tayari wataenda tu na yeye!.. kwasababu tayari Mungu kasema “atakuwa na wale wote wanaotoka kwenda kuhubiri”, hivyo Malaika wa MUNGU wataambatana na mtu huyo kuhakikisha kuwa watu wanapokea wokovu na ishara zinatendeka!.
Hizi ndio njia kuu mbili, zitakazowafanya Malaika wa Mungu, wafanye yale tunayoyataka au tunayofikiri, lakini si kwa kuwapa Amri, au kuwaamuru, wao wanafuata amri kutoka kwa Mungu na si kutoka kwetu. Sisi mamlaka tuliyopewa ni juu ya mapepo na falme zote za giza, kuziamrisha ziti chini yetu kwa jina la Yesu (Luka 10:19).
Kwa elimu Zaidi juu ya Malaika, wasiliana nasi inbox.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
Yohana mbatizaji alibatizwa na nani?
Je! baada ya ulimwengu huu kuisha malaika watakuwa na kazi gani tena?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.
Rudi nyumbani
Print this post
Ujumbe mzuri sana!naomba nipate somo hili zaidi kuhusu malaika na mungu awabariki kwa utendaji kazi wenu
We