Huyu Mkeni shemeji yake Musa alikuwa ni mtu wa namna gani? (Waamuzi 1:16)

by Admin | 4 July 2024 08:46 am07

Jibu: Turejee…

Waamuzi 1:16 “Hao wana wa Mkeni, HUYO SHEMEJI YAKE MUSA, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao”.

Wakeni walikuwa ni jamii ya watu waliokuwa wanaishi katika nchi ya “Midiani” (karibu na jangwa la Sinai).. Kwa urefu kuhusiana na waMidiani fungua hapa >>Midiani ni nchi gani kwasasa?.

Miongoni mwa hawa waMidiani ndiko alikotokea Babamkwe wake Musa aliyeitwa Yethro au jina lingine Rueli.. Huyu Yethro/Reueli ndiye aliyemzaa  Sipora aliyekuwa mkewe Musa.

Na huyu Yethro alikuwa na watoto wengine wa kiume mbali na wale mabinti wake saba tunaowasoma katika Kutoka 2:16, na mmoja wa mtoto wake wa kiume aliitwa “Hobabu” ambaye sasa “ndiye shemeji yake Musa (maana yake kaka yake Sipora, mke wa Musa)”.

Huyu Hobabu shemeji yake Musa alikataa kusafiri na wana wa Israeli, kwani wana wa Israeli walimtumaini yeye awatangulie njia kwani aliifahamu Zaidi, lakini alikataa kama maandiko yanavyosema..

Lakini maandiko mbeleni yanaonyesha alikubali, kwani uzao wake ulionekana ndani ya nchi ya Ahadi

Waamuzi 10: 28 “Ndivyo zilivyokuwa safari zao wana wa Israeli kwa majeshi: yao; nao wakasafiri kwenda mbele.

29 Kisha Musa akamwambia Hobabu, mwana wa Reueli Mmidiani, mkwewe Musa, Sisi twasafiri kwenenda mahali ambapo Bwana amenena habari zake hivi, Nitawapa ninyi mahali hapo; uje pamoja nasi, nasi tutakufanyia mema; kwa kuwa Bwana ametamka mema juu ya Israeli.

30 Naye akamwambia, Siendi mimi; ila nitairudia nchi yangu mwenyewe, na kwa jamaa zangu mwenyewe.

31 Naye akamwambia, Usituache, tafadhali; kwa kuwa wewe wajua jinsi tutakavyopanga nyikani, nawe utakuwa kwetu badala ya macho.

32 Itakuwa, ukienda pamoja nasi, naam, itakuwa mema yo yote Bwana atakayotutendea sisi, tutakutendea wewe vivyo

34 Na wingu la Bwana lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini.

35 Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema, Inuka, Ee Bwana, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao”.

Kwa funzo refu kuhusiana na habari hii ya Hobabu na Musa fungua hapa >>>>Kwanini Musa amtake Hobabu na tayari kulikuwa na Wingu linalowaongoza?

Kwahiyo huyu Hobabu ndiye aliyekuwa shemeji yake Musa na wanawe (yaani watoto wake) ndio hao wanaotajwa hapo katika Waamuzi 1:6 na Waamuzi 4:11 na pia wanatajwa katika sehemu mbali mbali za biblia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kuiaua Nchi ni kufanya nini? (Waamuzi 18:2).

BWANA NITIE NGUVU TENA. (Waamuzi 16:28)

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/04/huyu-mkeni-shemeji-yake-musa-alikuwa-ni-mtu-wa-namna-gani-waamuzi-116/