Waamuzi 16:28 “Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili”.
Samsoni haombi kujilipiza kisasi kwaajili ya Nywele zake zilizokatwa, bali kwajili ya “MACHO YAKE MAWILI”.. Maana yake macho yake yalikuwa ni bora kuliko nguvu zake… Laiti angeambiwa achague nguvu ziondolewe na macho yabaki, ni Dhahiri kuwa angechagua macho yabaki.. Na huo ungeweza kuwa uchaguzi wa kila mtu.
Macho ni Zaidi ya mikono, ni Zaidi ya miguu, ni Zaidi ya nguvu za mwili.. Na ndicho shetani alikitafuta kwa SAMSONI.. Macho yake!!!!… lakini ni jinsi gani angeyatoa?? Inahitajika kuziondoa kwanza nguvu zake za mwili.. Shetani alikuwa haziogopi nguvu za Samsoni, alichokuwa anakiogopa ni macho yake…
Kwani baada ya kumtoa macho alizitumia nguvu zake kusaga ngano za wafilisti…
Na leo hii adui anatafuta macho ya watu kama shabaha yake ya kwanza.. na macho anayoyatafuta si ya kimwili, bali yale ya kiroho..na anaanza kwanza kwa kudhoofisha nguvu za kiroho za mtu na kisha anamaliza kwa kumpofusha Macho ya kiroho … (hapo anakuwa amemaliza kazi!).. na hapo anaanza kumtumikisha kama alivyomtumikisha Samsoni.
2Wakorintho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
Lakini habari njema ni kwamba ipo NEEMA kuu juu yetu Zaidi ya ile iliyokuwa juu ya Samsoni. Kwani Samsoni alipomwomba Mungu amrejezee Nguvu zake alirejeshewa kweli na kuwaaharibu maadui zake lakini bado aliendelea kuwa kipofu..
Lakini katika wakati huu wa agano jipya tunaponyenyekea kwa Baba na kuomba msaada, kwa kumaanisha kabisa mbele zake, basi zile nguvu zetu adui alizoziteka zinarejea tena upya na pia macho yetu yanatiwa nuru.. Hiyo ndio faida ya kuwa ndani ya KRISTO.
Je nguvu zako za Kuomba zimeisha???, nguvu zako za kufunga zimeisha??..Nguvu za kumtumikia Mungu zimeisha??…. Kama ndio jua hiyo pia ni dalili ya kupofushwa macho na Ibilisi… Hivyo huwezi kuona mbele wala kutafakari yaliyopita… unahitaji msaada wa Mungu, kwa nguvu zako huwezi!!!
Huu ni wakati wa wewe kunyenyekea kwa Mungu kama Samsoni ili Bwana azirejeshe nguvu zako upya na macho yako yatiwe nuru.
Omba kwa kumaanisha, na ikiwezekana funga! Ili Toba yako iwe na nguvu.. Na matokeo utayaona!
Waefeso 1:18 “macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo”
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
KITENDAWILI CHA SAMSONI
UMEFUNULIWA AKILI?
BUSTANI YA NEEMA.
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
Rudi Nyumbani
Print this post