Maana ya Mithali 30:33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi

Maana ya Mithali 30:33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi

SWALI: Naomba kuelewa tafsiri ya mithali 30:32-33, isemayo;

Mithali 30:32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako. 

33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.

JIBU: Hekima inatueleza matokeo ya kila tendo linapofanyiwa kazi liwe ni zuri au baya litaleta majibu fulani tu. Hapa anatumia mfano wa siagi ambayo inatolewa katika maziwa.  Kwa kawaida siagi huwa imejificha ndani ya maziwa, hivyo ili kuipata tu ile siagi, ni kitendo cha kuipiga basi hutokea kwa juu yote,

Sasa kupiga hapo sio kuyachapa maziwa hapana, bali kuyakoroga, ndani chombo Fulani maalumu kwa muda mrefu, baadaye maziwa na siagi hujitenga vyenyewe.

Halikadhalika, pia damu huwa ipo ndani ya pua, lakini haiwezi kutoka yenyewe tu bila kuisumbua pua kwa kuipiga. Kwamfano mtu akikupiga ngumi ya pua ni wazi kuwa damu itatoka tu.

Ndivyo anavyofananisha na ugomvi, kwamba ni jambo ambalo lipo tu, wakati wowote katikati yetu. Mfano tu wa siagi ndani ya maziwa na damu ndani ya pua. Lakini mpaka ugomvi huo ujitokeze, unahitaji kuchochewa, kukorogwa, korogwa, kupigwa pigwa.

Anasema hasira inapoanza, aidha kwa kuzungumza maneno mabaya, mwenzako akakereka, haraka sana, weka mkono wako kinywani, usiendelee kuzungumza, kwasababu kitakachofuata ukiendelea sana ni ugomvi, yaani mapigano, na kudhuriana.

Mauaji, visasi, chuki, asilimia kubwa vimetokana na hasira zilizochochewa.

Lakini, uwezo huu wa kujizuia, una nguvu endapo mtu yupo ndani ya Kristo. Je! Umemwamini? Kama bado na upo tayari kumpokea leo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu chini.

Bwana akubariki

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?

Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments