SWALI: Kwanini Mungu aliufananisha uzuri wa Kaanani na kama nchi ibubujikayo maziwa na asali? Kwanini isiwe kitu kingine chochote, labda dhahabu na nafaka?
Kutoka 3:8 “nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi”.
JIBU: Mungu aliposema Kaanani ni nchi ibubujikayo maziwa na asali, hakumaanisha kuwa kuna mito ya maziwa, au mabomba ya asali, kila mahali hapana. Bali alitumia lugha hiyo ya picha kuonyesha uzuri wa nchi ile jinsi ulivyo.
Kama tunavyojua maziwa yanatolewa na mifugo, kama ng’ombe,. Na ng’ombe ili atoe maziwa mengi na ya kutosha, anategemea sana mazingira yenye malisho mazuri ya kijani na chemchemi nzuri za maji. Hivyo Hapo ni Mungu alikuwa anawaonyesha wana wa Israeli kuwa nchi waiendeayo si nchi kame, bali ni nchi yenye rutuba nyingi sana, ambayo mboga mboga na malisho mazuri vinastawi, kiasi kwamba tukisema ni maziwa basi mifugo yao itamwaga maziwa mengi sana, hadi yasiwatoshe kwa wingi wa malisho yaliyopo huko.
Vilevile aliposema asali, aliwalenga nyuki. Na nyuki ni wadudu wanaotegemea sana, aina mbalimbali za mimea na maua ili kutengeneza asali yao, Kama tunavyojua mahali ambapo pana jamii chache za miti na mimea, inawachukua muda mrefu sana kuunda asali kidogo, kwani inawagharimu kutembea umbali mrefu sana, kutafuta virutubisho hivyo.
Lakini kama wapo eneo lenye misitu, na jamii tofauti tofauti za miti na mimea, huwa inawachukua muda mfupi sana. Hivyo Mungu aliposema hiyo nchi ibubujikayo asali, alimaanisha kuwa ni nchi yenye aina mbalimbali ya miti ya vyakula na matunda, Kama tukisema ni nyuki watengeneze asali, basi asali itakuwa ni ya kumwagika sana.tofauti na hiyo nchi ya ukame waliyotoka.
Na ndio maana wale wapepelezi waliotumwa na Musa kwenda kuipeleleza Kaanani, aliporudi na kichala kikubwa cha mzabibu na tini na mkomamanga, waliwaambia wana wa Israeli maneno haya;
Hesabu 13:27 “Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake”
Unaona, kwa yale waliyoyakutana nayo huko walithibitisha maneno ya Mungu kuwa ni kweli, kuwa nchi hiyo ni ya maziwa na asali.
Hata sasa, Mungu ana mpango huo kwa watoto wake , kuwafikisha katika nchi hii, lakini ni lazima kwanza, awafundishe kanuni zake, na jinsi ya kuishi ndani yake. Vinginevyo wakiifikia na huku maisha yao bado hajabadilishwa, nchi hiyo itawatapika kama ilivyowatapika wenyeji wa Kaanani. Na kanuni zenyewe ni kuishi sawasawa na amri za Mungu (Neno lake).
Walawi 18:26 “Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ILI KWAMBA HIYO NCHI ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.
Walawi 18:26 “Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28 ILI KWAMBA HIYO NCHI ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.
Lakini tukiishi sawasawa na Neno lake, wakati huo utafika na Bwana atatuingiza katika nchi hiyo kama alivyofanya kwa wana wa Israeli walipozitii amri zake.
Hesabu 14:8 “Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UNYAKUO.
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
UFUNUO: Mlango wa 18
Kuota upo nchi nyingine.
ESTA: Mlango wa 4
Rudi nyumbani
Print this post
Shalom