Kwanini Musa amtake Hobabu na tayari kulikuwa na Wingu linalowaongoza?

by Admin | 4 July 2024 08:46 am07

Swali: Kwanini Nabii Musa amtake Hobabu (shemeji yake) kama dira yake ya kuelekea Kaanani na tayari Mungu alishawafunulia juu yao nguzo ya wingu wakati wa mchana na Nguzo ya moto wakati wa usiku kama dira yao na kama kitu cha kuwaongozea?


Jibu: Lipo jambo kubwa sana hapa la kujifunza..

Awali ya yote kama bado hujamfahamu Hobabu ni nani na inakuwaje awe shemeji yake Musa fungua hapa >>>Huyu Mkeni shemeji yake Musa alikuwa ni mtu wa namna gani? (Waamuzi 1:16)

Sasa kwa muhtasari ni kwamba kipindi wana wana wa Israeli wanatoka Misri kuelekea Kaanani, ni kweli Bwana aliwapa wingu na nguzo ya moto iwaongoze mchana na usiku.

Lakini Zaidi ya hayo Musa alitafuta tena mtu ambaye atamwongoza njia yao kuelekea nchi ya ahadi.. sasa swali ni alifanya makosa?… na tena akataka kumfanya kama “Macho” katika safari hiyo..

Waamuzi 10:28 “Ndivyo zilivyokuwa safari zao wana wa Israeli kwa majeshi: yao; nao wakasafiri kwenda mbele.

29 Kisha Musa akamwambia Hobabu, mwana wa Reueli Mmidiani, mkwewe Musa, Sisi twasafiri kwenenda mahali ambapo Bwana amenena habari zake hivi, Nitawapa ninyi mahali hapo; uje pamoja nasi, nasi tutakufanyia mema; kwa kuwa Bwana ametamka mema juu ya Israeli.

30 Naye akamwambia, Siendi mimi; ila nitairudia nchi yangu mwenyewe, na kwa jamaa zangu mwenyewe.

31 NAYE AKAMWAMBIA, USITUACHE, TAFADHALI; KWA KUWA WEWE WAJUA JINSI TUTAKAVYOPANGA NYIKANI, NAWE UTAKUWA KWETU BADALA YA MACHO.

32 Itakuwa, ukienda pamoja nasi, naam, itakuwa mema yo yote Bwana atakayotutendea sisi, tutakutendea wewe vivyo

34 NA WINGU LA BWANA LILIKUWA JUU YAO MCHANA HAPO WALIPOSAFIRI KWENDA MBELE KUTOKA KAMBINI.

35 Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema, Inuka, Ee Bwana, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao”.

Jibu ni La!.. Musa hakuwa Mjinga, wala hakuwa mtu wa kumtegemea Mwanadamu.. Daima alijua Mungu ndiye Ngao yake na watu wake, na wala hakuna mtu yeyote awezaye kumsaidia kazi.  Lakini Nabii Musa alifikiri Zaidi, Alijua watu aliona ni  watu wenye mioyo migumu, na shingo ngumu.

Alijua Imani yao kwa Mungu ilikuwa ni ndogo, na wengi wao ni watu wa mwilini, na alijua wasipopata mtu wa kuwapanga vyema kule nyikani, aliyemzoefu wa jangwa na njia, zitanyanyuka shida nyingi na hatimaye watamkufuru Mungu na kuadhibiwa wote.

Hivyo kwa faida ya watu wasiangamia aliwatafutia mwalimu wa mwilini ili awaongoze, na kuwafundisha jinsi ya kukaa jangwani, na hiyo ikawa dawa kwa sehemu kubwa sana.

Na utaona hii familia ya Yethro (babamkwe wake Musa na mashemeji zake), ilikuwa msaada mkubwa sana kiushauri katika safari ya wana wa Israeli jangwani na kwa Musa kwa ujumla. Kwani kipindi ambacho Musa alikuwa anawaamua watu wote peke yake kuanzia asubuhi mpaka jioni, alipokuja huyu babamkwe wake alimpa ushauri bora sana wa kuweka wakuu wa maelfu, wakuu wa mahamsini na wakuu wa mamia na wakuu wa makumi (Soma Kutoka 18:12-27).

NINI TUNAJIFUNZA KWA MUSA:

Musa alikuwa na “Macho juu” ambaye ni Roho Mtakatifu juu (kama wingu likimwongoza na watu wake) lakini pia alikuwa na “macho chini” (Hobabu, shemeji yake) kwaajili ya watu wake. Mambo haya yanaenda pamoja..

Wewe kwama Mzazi, unaye Roho Mtakatifu anayekuongoza wewe na familia yako kama Macho ya Juu, lakini hayo hayatoshi pekee, ni lazima watoto wako uwapatie waalimu watakaowafundisha njia za Roho Mtakatifu katika mashule yao waliopo, katika makanisa yao, katika shughuli zao n.k

Ukisema utawaacha na kuongozwa na Roho Mtakatifu kama wewe uongozwavyo, utawapoteza…wawekee waalimu.

Vilevile Mtumishi wa Mungu weka waalimu kwa watoto wako wa kiroho, weka wachungaji watakaowaangalia, itakuwa afya na heri kwao.

Bwana atusaidie

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

KAZI ZA ROHO MTAKATIFU

NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.

Je Musa kumwoa Sipora, Mkushi alifanya dhambi?

Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/04/kwanini-musa-amtake-hobabu-na-tayari-kulikuwa-na-wingu-linalowaongoza/