Mlango la kondoo ulikuwaje?(Yohana 5:2)

by Devis Julius | 6 July 2024 08:46 am07

Swali: Ule mlango wa kondoo unaotajwa katika Yohana 5:2, ulikuwa ni mlango wa namna gani?, na umebeba ujumbe au ufunuo gani sasa?


Jibu: Turejee.

Yohana 5:2 “Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano”.

Mlango wa kondoo unaozungumziwa hapo ulikuwa ni mlango mdogo katika Mji wa Yerusalemu, uliokuwa unatumika kupitishia kondoo kwaajili ya sadaka ya kuteketezwa (dhabihu).  Ulikuwepo mlango wa kuingilia watu na wa kuingizia wanyama ndani ya hekalu (katika Ua wa ndani).

Utaona lango hili linatajwa pia katika Nehemia 3:1, Nehemia 3:32 na Nehemia 12:39.

Nehemia 3:1 “Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga LANGO LA KONDOO; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli”

Lango hili la kondoo lilikuwa linamfunua BWANA YESU, kwani yeye mwenyewe katika Yohana 10:7 ametajwa kama LANGO LA KONDOO..

Yohana 10:7 “Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, MIMI NDIMI MLANGO WA KONDOO.

8  Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.

9  Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

10  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”

Kama vile ule mlango wa kwanza wa kondoo ulivyokuwa lango la yule aliyekuwa hawezi kwa miaka 38 kuponywa na Bwana YESU katika birika lile la Bethzatha vile vile  BWANA YESU ambaye ndiye LANGO halisi amebeba uponyaji wote wa roho zetu na miili yetu.

Je umempokea?

Kama bado fahamu kuwa upo katika hatari kubwa sana ya kuharibiwa na adui, kwani unakuwa upo nje ya zizi, ambapo yupo adui ambaye kazi yake ni kuchinja, kuharibu na kuua.

Yohana10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

10  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USIMZIMISHE ROHO.

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

JE! UNAMPENDA BWANA?

WALIKUWA WAMECHOKA NA KUTAWANYIKA KAMA KONDOO WASIO NA MCHUNGAJI.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/06/lango-la-kondoo-ulikuwajeyohana-52/