Je! Malaika wanazaliana?

by Admin | 24 July 2024 08:46 am07

Wapo wanaodhani kuwa malaika wanao uwezo wa kuzaliana sawasawa na habari ya wana wa Mungu na binti za wanadamu inayozungumzwa  katika kitabu cha Mwanzo.

Mwanzo 6:1-3,  Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Kwa habari hiyo wengi hufikiri, hao wana wa Mungu walikuwa ni malaika, ukweli ni kwamba hawakuwa malaika bali wanadamu. Yesu alisema, tutakapofika mbinguni, hatutaoa wala kuolewa, tutafanana na malaika, Kuonyesha kuwa malaika hawazaliani. (Mathayo 22:30)

Vilevile katika habari hiyo hatuoni kwamba malaika wakiadhibiwa, bali wanadamu, kuonyesha kuwa ni jambo la kibinadamu. Kwa urefu wa fundisho hilo, fungua hapa >>> WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.

Viungo vya uzazi viliumbwa mahususi kwa viumbe wa ulimwenguni, kwa lengo la kuijaza nchi. Lakini vya mbinguni havikuumbwa kwa utaratibu kama huu wa kwetu.

Hivyo kwa hitimishi ni kuwa malaika watakatifu hawazaliani. Kwasababu wao ni viumbe vya rohoni, waishio milele. Hivyo hawahitaji kuzaliana.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?

Je malaika wote wana wabawa?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/24/je-malaika-wanazaliana/