Katika maandiko tunaona, Malaika wakionekana kwa mifano ya viumbe mbalimbali vya duniani, ikiwemo wanadamu. Kwamfano wale wenye uhai wanne, wapo waliokuwa na uso kama wa tai, wengine simba, wengine ndama na wengine wanadamu(Ufunuo 4:7). Maserafi na Makerubi walionekana kuwa ni malaika wenye mabawa. (Kutoka 25:20, Isaya 6, Ezekieli 10).
Lakini wapo pia walionekana kwa mfano wa wanadamu kabisa, mfano wa hawa ni wale waliomtembelea Ibrahimu wakala naye, kisha wakaenda Sodoma. (Mwanzo 18 &19)
Kwahiyo si malaika wote waliokuwa na mwonekano wa mabawa. Lakini ni vema kufahamu kuwa mabawa au mionekano si vitu ambavyo vinawafanya watembee au wawe na uwezo ule, wale ni viumbe vya rohoni hivyo hawategemei kanuni za kidunia kutembea, ijapokuwa wataonekana kama wanadamu bado sio wanadamu, hawawezi kuzaliana, wataonekana na mifano ya ndege sio ndege wala akili zao hazipo vile.
Kwahiyo kujua kama malaika wote wana mabawa au hawana, si muhimu. Muhimu ni kufahamu ni kwamba wamewekwa kutuhudumia sisi tutakaourithi wokovu. Hivyo tumtiipo Kristo maana yake ni tunaruhusu huduma yao kutenda kazi katikati yetu, hapa ulimwenguni.
Waebrania 1:13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Lakini kinyume chake ni kweli umtiipo shetani, tafsiri yake ni kuwa unayaruhusu mapepo kufanya kazi hapa duniani.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MALAIKA NI WALIMU WA SIFA KWETU, TUJIFUNZE KWAO!
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
(Opens in a new browser tab)HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.(Opens in a new browser tab)
Rudi Nyumbani
Print this post