by Admin | 30 July 2024 08:46 am07
SWALI: Maandiko yanaposema Habili ijapokuwa amekufa angali akinena, je! Ananenaje, wakati yeye ni marehemu. Je! Hiyo inamaana wazee wetu wa zamani wanaweza kunena na sisi?
Waebrani 11:4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena
JIBU: Kibiblia ni kweli kabisa watakatifu waliokufa kale hunena nasi. Lakini kunena kwao ni tofauti na huku kunakodhaniwa, kwamba mzimu unakutokea kwenye ndoto, au unasikia sauti ya petro makaburini ikizungumza na wewe, Hapana, ukiona hivyo ujue huzungumzi na huyo mtu, bali ni pepo.
Sasa watakatifu waliokufa wanazungumzaje na sisi?
Ni kwa ushuhuda waliouacha. Maisha yao na maagizo yao, ndio huzungumza nasi, sikuzote, kana kwamba tupo nao sasa, kwa mafundisho yao yaliyopo mpaka sasa kana kwamba tunawaona wenyewe kumbe wamekufa.
Ndio maana ile habari ya Yule tajiri wa Lazaro, tunaambiwa alipofika kule kuzimu akaomba mtu atolewe kwa wafu awahubirie injili, akakataliwa, kuonyesha kuwa hakuna mtu aliyekufa mwenye uwezo wa kuja tena kuzungumza na sisi, nafasi hiyo haipo kwao. Lakini waliambiwa WANAO MUSA NA MANABII, WAWASIKILIZE.
Luka 16:29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
Maana yake ni kuwa sio kwamba Musa kweli alikuwepo duniani, au manabii wa kale kama Isaya walikuwa duniani kwa wakati huo, anaambiwa hayo maneno. Lakini shuhuda zao na mahubiri yao, huwawakilisha wao. Tunaweza kusema “ijapokuwa wamekufa wangali wakinena”
Ndivyo ilivyo kwa Habili, ijapokuwa aliuliwa na ndugu yake, lakini IMANI yake inasema nasi mpaka leo. Mitume wa Kristo ijapokuwa hawapo duniani lakini sauti zao tunazisikia hadi sasa.
Lakini pia kuna mahali pengine biblia inasema damu ya Yesu hunena mema kuliko ya Habili (Waebrania 12:24). Kufahamu kwa kina damu ya mtakatifu hunenaje? Pitia somo hili. >>> DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
Rudi Nyumbani
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/30/ijapokuwa-amekufa-angali-akinenawaebrania-114/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.