by Admin | 30 September 2024 08:46 am09
Swali: Kucheza Magemu kwenye komputa au simu ni sahihi? Mfano magemu ya mpira, vita, kupigana, karata, magari, pool-table, zuma, na mengineyo ni dhambi?..
Jibu: Kabla ya kujibu swali hili, ni muhimu kwanza kujua michezo hiyo kama ni sahihi kuishiriki au la!
Awali ya yote mkristo aliyeokoka, hapaswi kushiriki michezo ya kupigana, iwe awanjani (ndondi) au vitani (iwe kwa nia ya kifursa au burudani) kwasababu biblia inasema kushindana kwetu si juu ya damu ya nyama bali juu ya falme na mamlaka za mapepo katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:10-13 na vita vya kiroho dhidi ya mapepo si vya kujiburudisha au kujifurahisha).
Vile ile mkristo hapaswi kucheza pool-table kwasababu ni mchezo wa ibilisi na unaochezwa na watu wasio na Roho wa Mungu.. ndio maana meza zake zipo maeneo yafanyikapo anasa kama disko, au bar… huwezi kukuta poo-table kanisani.
Vile vile mkristo hapaswi kushiriki michezo mingine yote ya kidunia iliyojishonesha na mifumo ya kidunia ikiwemo mipira na basket.
Sasa kama hapaswi kushiriki wala kushabikia michezo hiyo, vile vile Magemu yanayoshabikia mambo hayo hapaswi kushiriki, kwasababu hakuna tofauti ya kushabikia ukiwa uwanjani na kucheza magemu yake.. (kwasababu ile shangwe unazaliwa moyoni kutokana na kile unachokiona au kishiriki).
Hivyo si sahihi kwa mkristo kucheza magemu katika kompyuta au simu au katika kifaa kingine chochote ikiwemo PS (Play station).
Lakini yapo magemu yaliyotengenezwa pasipo kuhusisha michezo ya damu na nyama, (hayo ndio hatari kabisa) kwasababu yamebuniwa kutoka katika mambo yanayoendelea rohoni.
Kwamfano utaona kuna magemu ya Nyoka,.. joka linazunguka na kumeza vitu, sasa mambo haya hayapo katika ulimwengu wa mwili, lakini yapo katika ulimwengu wa roho.. sasa kwasababu shetani anataka kuendeleza mahusiano kati yake na wanadamu kwa hata njia ya mwili, ndio yanakuja haya magemu.
Mtu anapocheza game la kumwongoza nyoka kumeza vitu, au anapocheza game la kukumbizwa na joka, au kukimbizwa na viumbe visivyojulikana, basi anashiriki basi anathibitisha mambo hayo katika roho, na hivyo maisha yake yataendeshwa na hayo maroho kwa kupenda au kutokupenda. (Hata ndoto zake zitakuwa zimejaa hayo mambo).
Roho ya kupenda na kucheza magemu inaongezeka kwa kasi siku hizi za mwisho, na hasa kwa njia ya simu.. zamani ilikuwa ni agenda ya kupanda msingi wa maroho kwa watoto, lakini siku hizi hata watu wazima, hivyo ni kuongeza umakini sana.
Biblia inasema tusiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani, kwani mtu akiipenda dunia hata kumpenda Baba hakupo ndani yake.
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”
Na tena inasema yoyote yaliyo yenye kupendeza na yaliyo ya staha na kweli tutayafakari hayo (Wafilipi 4:8)
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.
Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
Je kumwimbia Mungu kwa kucheza ni sahihi kibiblia?
Jicho kucheza ni ishara ya nini?
Je! Kushiriki au kujihusisha kwenye michezo ni dhambi?..
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/09/30/je-kucheza-magemu-ni-sahihi-kwa-mkristo/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.