by Admin | 7 October 2024 08:46 am10
Swali: Biblia inasema tumepewa mboga za majani kuwa chakula chetu, na Bangi pia ipo miongoni mwa zao la mboga za majani…sasa kwanini iwe dhambi kulitumia kama mboga au kiburudisho cha kusisimua (kuvuta) na ilihali ni Mungu mwenyewe ndio kaumba?
Jibu: Turejee..
Mwanzo 9:3 “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa MBOGA ZA MAJANI, kadhalika nawapeni hivi vyote”.
Ni kweli maandiko hayo yanathibitisha ulaji wa mboga, lakini si mboga zote!.. Tukisema kila mboga iliyopo kondeni tumepewa tule, tutakuwa hatujayaelewa vizuri maandiko kwasababu kuna mboga nyingi sana ambazo sumu!, ambazo zinamwonekano mzuri lakini hazifai kwa chakula… na Mungu hawezi kumpa ruhusa Mtu wake aliyemuumba, ale SUMU!..
Zipo mboga kwaajili ya chakula cha wanadamu, nyingine kwaajili ya wanyama na hazifai kwa wanadamu… vile vile zipo mboga zisizofaa kwa chakula cha wanadamu na wanyama… Mboga hizo zinabaki tu kwa utukufu wa Mungu, au kwaajili ya urembo, mfano wa mboga hizo ni MAUA.
Kuna Maua ambayo yana mwonekano mzuri sana lakini ni SUMU kali sana, mfano wa hayo ni kama haya yanavyoonekana hapa chini.
Hayo ni mfano wa Mboga, lakini si kwaajili ya kula bali kwaajili ya urembo tu.. yameumbwa na Mungu kwa lengo hilo, hivyo mtu akila hayo anaweza kupata madhara makubwa ya kiafya au hata kifo.
Vile vile na Bangi, inaweza kuwepo katika kundi hilo la MAUA, kama itatumika kwa urembo si vibaya, lakini kwa matumizi mengine ya ndani ya mwili wa binadamu ni hatari.
Kwahiyo si kila kilicho halalishwa basi kinafaa kwa matumizi yote.. hapana!.. Mboga zimehalalishwa lakini si kwa matumizi ya chakula tu, ndivyo maandiko yanavyotufundisha..
1Wakorintho 10:23 “Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo”.
Kwahiyo ulaji, au uvutaji wa Bangi ni dhambi kibiblia, vile vile matumizi ya tumbaku kula au kuvuta ni dhambi, kwani miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na tena maandiko yanasema mtu akiliharibu hekalu hilo Mungu naye atamharibu mtu huyo (Soma 1Wakoritho 3:16-17 na 1Wakorintho 6:19).
Na Bangi inaharibu ufahamu wa mtu, ambao ndani yake kunazalika hasira, kutokujali, vurugu, matukano, mauaji, uasherati na mambo yote mabaya..
Hivyo Bangi ni haramu, vile vile tumbaku na mazao mengine yaletayo matokeo kama hayo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nyungu ni nini kibiblia?(Ayubu 41:20,31, Waamuzi 6:19)
JE UNAZAA MATUNDA NA KUWAPONYA MATAIFA?
WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.
Nini maana ya mmoja alikufa kwaajili ya wote hivyo walikufa wote? (2Wakorintho 5:14)?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/10/07/kama-ni-mungu-ndiye-kaumba-zao-la-bangi-kwanini-tena-iwe-dhambi-kuitumia/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.