Hii ni maana ya Mathayo 6:29 hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo

by Admin | 14 October 2024 08:46 am10

SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya vifungu hivi; 

Mathayo 6:29

[29]nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.


JIBU: Katika habari hiyo Mungu anaeleza jinsi anavyoweza kutujali na kututunza sisi kipekee kwa uweza wake wa ki-Mungu, akifananisha na jinsi anavyoyatunza maua yake ya kondeni ambayo leo yapo kesho yananyauka na kutupa tanuruni.

ndio hapo anasema tusiwe na shaka ya leo tuvae nini,  kama Mungu anayavika vizuri maua hayo ambayo ni kwa muda mfupi tu huchanua baadaye hunyauka, si zaidi sisi tulio na thamani nyingi zaidi ya hivyo vyote?

Tena anasisitizia hata Sulemani katika fahari yake yote, hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya maua hayo.

Kumbuka Sulemani alikuwa ni mtu tajiri sana, mavazi yake yalikuwa ni ya thamani sana, lakini yalitegemea kuchovywa na kurembwa kwa rangi mbalimbali, ambazo hizo baada ya kipindi fulani hupauka au kuchuja.

Lakini maua hayapakwi rangi bali uzuri ule ni rangi yao kwa asili itokayo ndani. hayafifi rangi. Sulemani hakuwahi kuwa na vazi la namna hiyo.

Isitoshe maua nayo licha ya kuwa na mwonekano mzuri lakini pia hutoa harufu yao nzuri ya asili, kitu ambacho hawezi kukiona kwenye vazi la aina yoyote zuri duniani kutoa harufu yake yenyewe, yanategemea kupuliziwa marashi.

Hivyo hiyo ni kutufundisha kuwa Mungu anaweza kutunawirisha na kutupendezesha zaidi ya matarajio yetu, lakini hiyo hutimia kwanza pale tunapojishughulisha  na mambo ya ufalme wake, ndio hayo mengine sasa ya chakula na mavazi atuzidishie.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ONA FAHARI JUU YA BWANA.

Nyinyoro ni nini?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/10/14/hii-ni-maana-ya-mathayo-629-hata-sulemani-katika-fahari-yake-yote-hakuvikwa-vizuri-kama-mojawapo-la-hayo/