KILA MTU NA AMCHE BABA YAKE NA MAMA YAKE.

by Admin | 5 February 2025 08:46 am02

(Mafunzo maalumu kwa watoto na walezi).

Kama wewe ni mtoto basi jifunze haya, na kama ni mzazi basi pia jifunze haya na pia mfunze mwanao…

Mambo ya Walawi 19:3 “Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu”

Biblia imetumia neno “kumcha” kuonyesha msisitizo wa jambo hilo, jinsi lilivyo la msingi.

“Kumcha mzazi” sio “kumwabudu” bali ni kumpa heshima ya hali ya juu sana, ikiwemo kumsikiliza, kumtii na kufanya yale anayosema bila kumsumbua sumbua ikiwa jambo hilo si nje na mapenzi ya MUNGU.

Maana yake kama tunavyomcha MUNGU, kila atuambiacho tunakizingatia, kwasababu tunajua kwake kuna baraka na laana, kadhalika na wazazi hivyp hivyo wanaweza kutubariki na kutulaani.

Sasa wengi wetu inapofika eneo hili la kutafakari mzazi na mtoto akili zetu huwa zinalenga kufikiri wale watoto walio chini ya malezi ya wazazi, pasipo kujua kuwa hata uwe na miaka 70 na kama mzazi wako yupo hai bado hiyo amri inakuhusu hata wewe ya kumcha mzazi wako, kwani wewe bado ni mtoto kwake.

Amri ya watoto kuwatii na kuwaheshimu wazazi inawahusu hata wenye ndevu na hata wazee wenye mvi, haijalishi wewe sasa ni bibi au babu na unao wajukuu…kama mzazi wako yupo hai unayo amri ya kumcha..

Lakini ukimvunjia heshima mzazi kwasababu ni mzee, basi fahamu kuwa bado hujayajua maandiko.

Mithali 23:22 “Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee”

Jifunze kumcha Mzazi, wapo watu wanapambana na wazazi wakati wote, wanagombana na wazazi, na hata kuwaita wachawi, usiwe jamii ya hao watu waliotabiriwa..

Mithali 30:11,”Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao”. 

Yafuatayo ni madhara machache ya kutomcha Mzazi.

    1. Jicho kung’olewa.

Mithali 30:17 “Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa Na vifaranga vya tai watalila”

Mtu aliyetolewa macho ni kipofu, hawezi kuona ya mbele wala ya nyuma katika maisha yake, atabaki anapapasa tu.

  2. Kifo.

Mithali 20:20 “Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu”.

Maana ya Taa kuzimika ni “kifo”. (Soma Ayubu 21:17).

Yapo na madhara mengine mengi ikiwemo kukosa Heri mashani..

Je unamcha mzazi wako?..je unameombea?..je umepatana naye?. Kama bado hujafanya hayo yote basi anza leo.

Bwana akubariki na atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/02/05/kila-mtu-na-amche-baba-yake-na-mama-yake/