by Devis | 26 June 2025 08:46 pm06
SWALI: Yesu alikuwa na maana gani aliposema ‘tena siku ile hamtaniuliza neno lolote ’
Kwanini ajiangue kwa namna hiyo angali yeye ndiye mwokozi wa kutegemewa kila kitu?
Yohana 16:23
[23]Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
JIBU:
Kama tunavyojua hakukuwahi kutokea kiongozi aliyekuwa na matokeo makubwa duniani kama Yesu Kristo.
Namna ya uongozi wake, Kwa jinsi ulivyokuwa thabiti na bora Matokeo yake ndio tunayoana mpaka sasa duniani kwenye imani.
Hivyo maisha yake na huduma yake sio tu vinatufundisha njia ya wokovu lakini pia vinatufundisha namna kiongozi bora anavyopaswa Awe.
Matokeo Ya mitume wake kuwa nguzo kwa makanisa ya vizazi vyote ni matokeo ya namna ambavyo alivyowakuza anawakuza.
Bwana Yesu hakutengeneza Wafuasi, bali alitengeneza watu kama Yeye…Na hivyo katika kuwafundisha wanafunzi wake aliwakuza Ki vitendo zaidi kuliko maneno ya vitabu vingi vya kidini na mapokeo.
Kwamfano utaona kuna mahali anawatuma wawili waenda kuhubiri injili mahali ambapo angepaswa kwenda yeye mwenyewe, lakini aliwaacha waende.
Luka 10:1
Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.
Mahali pengine aliwaacha watoe pepo na waliposhindwa hakusema ‘wanangu nyie ni wachanga, basi nitakuwa nawasaidia tu’…hapana Kinyume chake aliwakemea Kwa upungufu wa imani zao.
Vivyo hivyo katika tukio hili, wanafunzi wake walitarajia kila siku watakaa naye wamuulize maswali yeye, kisha awajibie kutoka kwa Baba.. Ni sawa na mtoto mchanga ambaye kila siku anasubiria atafuniwe tu chakula apewe…unadhani hilo litaendelea sana?
Vivyo hivyo hilo halikuwa lengo la Bwana Yesu, bali alitaka kuwafundisha kanuni za wao wenyewe kumuuliza Mungu na kujibiwa moja kwa moja kama yeye alivyokuwa anajibiwa…
Na njia moja wapo ilikuwa ni yeye kuondoka, kisha kwa kile kitendo cha wao kumkosa Bwana wa kumuuliza, wajifunze kuomba kisha Roho ajae ndani yao, ndipo waanze sasa kupokea mafunuo ya kweli na ujasiri kutoka kwa Mungu..
Lakini pia waombe jambo lolote kwa jina la Yesu, wapokee mahitaji yao. Na Kweli mambo hayo yalianza Kutokea baadaya ya Pentekoste.. wote walikuwa ni kama ‘Yesu-dunia’ hakuna hata mmoja alifikiri au kuwaza kwamba kuna umuhimu tena wa Yesu kutembea nao, kimwili bali waliweza kuyafanya yote.
Hiyo ni tabia ya kiongozi bora…huwafanya wanafunzi wake kuwa kama yeye, na wakati mwingine kutenda hata zaidi ya yeye…Yesu aliwainua zaidi kwa kusema.
Yohana 14:12
[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Hiyo ndio sababu kwanini aliwaambia hayo maneno.
Yohana 16:23-24
[23]Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Hata sasa Bwana anataka kuona ukomavu kama huu ndani ya maisha ya wakristo wengi.. Ikiwa kila siku utakuwa unategemea Mchungaji wako akuombee, ni lini utaweza wewe mwenyewe kuomba na kuwaombea wengine? Sababu ya watu wengi kutojibiwa maombi yao na Mungu ni hiyo.. Ameshakomaa kiroho, Mungu anaona anaouwezo wa kupambana na tatizo yeye mwenyewe, atataka kiongozi wake amsaidie..
Hicho kitendo kinapunguza utendaji Kazi wa nguvu za Mungu, kwasababu yeye hataki tumgeuze mwanadamu Mungu..Ukiokoka, fahamu kuwa Roho Mtakatifu yupo ndani yako, na kuanzia huo wakati na kuendelea unawajibu wa kuufanyia mazoezi wokovu wako, jifunze kuomba mwenyewe, jifunze kuombea watu, soma biblia mwenyewe Mungu akufundishe..
Hizo ndio hatua bora za ukuaji kiroho.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/06/26/yesu-alikuwa-na-maana-gani-aliposema-tena-siku-ile-hamtaniuliza-neno-lolote-yohana-1623/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.