Je kuna andiko linalomruhusu mwanamke kuwa sister?

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Nadhani utakuwa unazungumzia ma-sisters mfano tunaowaona katika  dini ya Kikatoliki. Ni wazi kuwa hakuna andiko lolote au mahali popote kwenye biblia linasema hivyo. Lakini mwanamke anaweza akajizuia asiolewe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, biblia imesema hivyo katika

1Wakorintho 7: 34 “Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane”.

Hivyo mwanamke yeyote anayejizuia kuolewa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, hafanyi vibaya kulingana na maandiko lakini amaanishe kweli kufanya hivyo vinginevyo kama atakuwa anaishi kwa kulipuka tamaa, basi atakuwa anajitafutia mwenyewe hukumu..

Pia lipo andiko lingine linasema..

1 Timotheo 4 :1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wenginewatajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3WAKIWAZUIA WATU WASIOE, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

Unaona hapo inasema “wakiwazuia”..ikiwa na maana kuwa wanahaja ya kuoa lakini wanalazimishwa kufanya hivyo kutokana labda na utaratibu wa dini zao au madhehebu yao..kwamba ili wapewe nafasi fulani inawapasa wawe hivyo…lakini haimaanishi kuwa mtu yeyote ambaye ametaka kumtumikia Mungu pasipo kuoa au kuolewa anakwenda kinyume na maandiko.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA.

MARIAMU

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

RABONI!

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/je-kuna-andiko-linalomruhusu-mwanamke-kuwa-sister/