Je! mabalasi Bwana Yesu aliyoyatumia kugeuzia maji kuwa divai, yalitumika tu kwa kazi hiyo?

by Admin | 3 September 2019 08:46 am09

SWALI: Shalom Wapendwa Samahani Nilikuwa Nauliza Katika Kitabu Cha Yohana 2:1 Na Kuendelea Katika Harusi Ya Kana Yesu alitumia “MABALASI ile Mitungi Ya Kujitawadhia kugeuza maji kuwa Divai, swali linakuja je? ilikuwa ni kawaida kutumia hiyo mitungi kuwekea divai au kulikuwa na vyombo vingine.


JIBU: Mabalasi vilikuwa ni vyombo maalumu vya kuhifadhia vitu…Ni kama leo tuseme mapipa!..unaweza kwenda mahali ukakuta nyumba moja pipa wanalitumia kuwekea maji ya kunywa, pengine wanawekea mbegu za mazao, mahali pengine wanatumia pipa kuhifadhia pombe wanazotengeneza, sehemu nyingine wanatumia kuwekea maji ya kwendea bafuni n.k Na hapo katika habari hiyo, Mabalasi ni kama mapipa, isipokuwa hapo yalitumika kwa kutawadhia. Na kutawadha kunakozungumziwa hapo, sio kule kwa chooni, bali ni kule mtu anapojisafisha sehemu baadhi za mwili kama mikono na miguu…kabla ya kuingia kwenye Ibada, hiyo ilikuwa ni desturi za Wayahudi,…Na ilikuwa mtu hajisafishi ndani ya hilo balasi, hapana! Bali anachota maji kutoka kwenye hilo balasi na kujisafisha kando…

kama Bwana Yesu alivyowatawadha wanafunzi wake miguu kabla ya kushiriki meza ya Bwana (soma Yohana 13:1-18)…Hivyo mabalasi hayo ya kutawadhia vilikuwa ni vyombo visafi na si vichafu. Na kwanini Bwana Yesu aliagiza yatumike hayo Mabalasi na si vyombo vingine?…Ni kwasababu ndio vyombo pekee vilivyokuwa karibu na pale alipo (maeneo yale) na vilikuwa tupu

Yohana 2:6 “Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu”.

Ni kama tulivyosema, pipa hilo hilo linaweza kutumika kuhifadhia pombe, na pipa hilo hilo linaweza kutumika kuhifadhia maji, au mazao au taka, n.k…. Hivyo kama biblia inavyotuambia hapo mabalasi hayo yalitumika kwa ajili ya kutawadhia…lakini Bwana Yesu alilyaona yanaweza kufaa pia kwa kuwekea divai, ndipo akageuza maji yale kuwa divai ndani ya mabalasi yale, na watu walikunywa bila kuona shida yoyote wala kinyaa..kwasababu pengine ilishazoeleka na ilikuwa inajulikana kuwa mabalasi pia yanatumikaga kwa shughuli za kuhifadhia Divai ..

 Ubarikiwe!


Mada Nyinginezo:

MATUMIZI YA DIVAI.

JE! ULEVI NI DHAMBI?

MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.

NJAA ILIYOPO SASA.

UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?.

MSTARI HUU UNA MAANA GANI? “TUPA CHAKULA CHAKO USONI PA MAJI; MAANA UTAKIONA BAADA YA SIKU NYINGI”. (MHUBIRI 11:1)


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/03/je-mabalasi-bwana-yesu-aliyoyatumia-kugeuzia-maji-kuwa-divai-yalitumika-tu-kwa-kazi-hiyo/