Mungu anasema hatagharikisha dunia na maji tena,.Kwanini watu wanasema dunia itaangamizwa?

by Admin | 3 September 2019 08:46 am09

SWALI: Shalom watumishi wa Mungu Leo nina swali nataka niulize maana linanitatiza jambo hili ni kutoka kitabu cha Isaya. 

Isaya 54:9 “ Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.

10 Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye”

 Je! swali lina kuja hivi mtumishi Leo hii kuna watu nimewaskia wakisema hakuna ghadhabu ya Mungu tena mana amekwisha sema maji ya Nuhu hayatapita tena na tunajua maji ya Nuhu ilikua ni siku ya mwisho ya dunia je! ni kweli Mungu hata shusha hasira yake tena? kuna watu wana sadiki kujitetea na maovu yao kupitia neno hli wakisema hakuna hukumu tena maana Mungu amekwisha apa!


JIBU: Shalom! Ni kweli Mungu hataingamiza dunia tena kwa maji, kama Neno lake hilo linavyosema hapo juu! Lakini hiyo haimaanishi kuwa dunia haitaangamizwa, itaangamizwa lakini sio kwa maji, bali na kwa kitu kingine, kwasababu Neno linasema kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu (yaani siku za mwisho) kwahiyo kama siku za Nuhu ulimwengu uliangamizwa kwa maovu yake, kadhalika na siku hizi za mwisho ulimwengu utaangamizwa vile vile kwa maovu yake..lakini si kwa maji. Na kama si kwa maji basi ni kwa kitu gani?…Jibu lipo kwenye biblia hiyo hiyo..tusome:

 2 Petro 3:5 “Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu” 

Kwahiyo siku sio nyingi dunia hii itakwenda kugharikishwa KWA MOTO!..Usidanganyike hata kidogo kuwa hakuna hukumu inayokuja!..Hukumu ni lazima ije kwasababu Mungu alishasema ni lazima ije!..Hivyo ni kuwa macho na kukesha katika roho ili siku hiyo isitujie kama mwivi. 

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

PEPETO LA MUNGU.

LAANA YA YERIKO.

BIDII YA MFALME YOSIA.

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/03/mungu-anasema-hatagharikisha-dunia-na-maji-tena-kwanini-watu-wanasema-dunia-itaangamizwa/