by Admin | 14 October 2019 08:46 pm10
Freemason ni nini? nini historia ya freemason?, nani mwanzilishi wa freemason na Je! Freemasons ni wa kuogopwa? Masharti ya freemason ni yapi?
Shalom! Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuongeze maarifa ya Neno la Mungu.
Leo tutajifunza juu ya kikundi kinachoitwa “Freemasons” na jinsi gani ya kutoka au kuwasaidia ambao tayari wameshaingia humo.
Kwa kuanzia tujifunze kidogo historia ya kikundi hicho: Freemasons tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni “wajenzi huru” ingawa hawatambuliki kwa jina hilo, lakini kwa asili ni kikundi cha wajenzi. Kikundi hichi kilianzishwa miaka mingi kinadai tangu wakati wa ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani, japo umaarufu wake umekuja kuwa mwingi katika karne za hivi karibuni.
Kikundi hichi kinaamini “kulikuwa kuna siri zimefichika ambazo ndizo zilitumika katika ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani”...Na kama vile wakristo wanavyoamini kuwa Yesu Kristo ndiye Masihi na kiini cha siri zote za Mungu. Vivyo hivyo Na Freemasons wenyewe wanamwamini mtu mmoja anayeitwa HURAMU, Kama Masihi wao, huyu anapatikana katika kitabu cha 1Wafalme 7, ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa mji wa Tiro ambao kwa sasa ni maeneo ya nchi ya Lebanoni. Huyu ndio kama Masihi wao, Na Mwanzilishi wa freemasons kulingana na wao.
JE FREEMASONS NI KIKUNDI CHA SIRI?
Sasa kikundi hichi ni cha Siri, tukisema ni cha siri haimaanishi watu wake hawaonekani, au majengo yao hayajulikani..Hapana! Vikundi vya Freemasons vyote vimesajiliwa na serikali zote duniani, na vinalipa kodi, kwahiyo ni watu waliowazi..Kitu pekee ambacho ni siri ni “IBADA ZAO”. Na sheria za dunia zinawalinda kufanya ibada zao kwa siri. Kama vile sheria zinavyolilinda shirika la COCACOLA kuficha formula ya utengenezaji wa vinywaji vyao.Ni watu wachache sana wanafahamu, Na hiyo yote ni kuzuia unakiliji wa bidhaa zao.(www.wingulamashahidi.org)
Freemasons ina wanachama zaidi ya milioni 6 duniani kote, miongoni mwao wakiwa, maraisi, wanasiasa, wana uchumi, wanasayansi, madaktari, waalimu, viongozi wa dini, wakulima, n.k…Idadi kubwa ya wanachama hao ipo nchini Uingereza na Wales.
Mshirika kabla ya kujiunga ni lazima awe ana imani ya kuwa kuna “nguvu ya Kiungu”….Hiyo ikifunua kwamba tayari hicho ni “kikundi cha rohoni” kama huamini huwezi kuwa mshirika …Wanaojiunga huko ni watu kutoka dini zote duniani, waislamu, wahindu, wakristo-jina, wabudha n.k..Baada ya mshirika mpya kujiunga anatakiwa kukusanyika na wenzake mara kwa mara katika majengo yao maalumu ya ibada yanayoitwa “Grand Lodges”..Na wanawake hawaruhusiwi kujiunga katika kikundi hicho.
Ndani ya Ibada hizo kwenye majengo yao wanatumia ishara ya vitu vingi, katika vidole, mikono, miguu, na pia wana ishara za picha na vito kama pete, mikufu, stika, ribbons, na ishara za vifaa vya ujenzi kama bikari, rula, pembe tatu.n.k na Kila ishara ina maana yake. Kama vile sisi wakristo tunavyokuwa na ishara ya misalaba kanisani mwetu, Inafunua kitu kilichotendeka Kalvari.
Sasa Ibada hizo zinabadilika kulingana na vyeo, wenye vyeo vya chini hawafanyi ibada zinazofanana na wenye vyeo vya juu, na pia wenye vyeo vya chini hawafahamu siri nyingi kama wanazofahamu wenye vyeo vya juu. Hapa ndipo watu wengi wasipojua!…tutakuja kupaelewa vizuri mbele kidogo mwa somo hili…
Sasa vyeo hivyo vimegawanyika katika ngazi kuu 33 wanazoziita “shahada” au “degrees”
Mshirika mpya anayejiunga, kuna viapo anaambiwa aape, moja ya viapo hivyo ni kukiri kuwa mwaminifu, na kutokufichua siri yoyote ya chama hicho, na pia ataambiwa akiri kwamba endapo atafichua basi atakufa, na pia anaambiwa aape kwamba atakuwa mwaminifu, na pia atakuwa tayari kushirikiana na wenzake, na kusaidiana na wenzake kwa hali na mali…(www.wingulamashahidi.org)
Na katika hatua za awali, ataambiwa tu hicho ni kikundi cha kijamii!, kinachoamini katika ujenzi, na cha kusaidiana, na wala hataambiwa siri nyingi za kikundi hicho,..Na wala hawatamkataza kurudi kusali katika kanisa lake kama ni mkristo. Ila kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda na anayozidi kupanda vyeo, ndipo ataanza kugundua kuwa sio sehemu ambayo aliambiwa pindi alipokuwa anajiunga.
Wengi waliojiunga na kutoka wanasimulia…”kuwa pindi walipojiunga, hawakujua chochote na pia walikuwa wanauhuru wa kuendelea kurudi kwenye makanisa yao kuabudu” na tena walikuwa wanapingana vikali na wale waliokuwa wanakishutumu chama hicho kuwa ni chama cha kishetani” na kinachoamini mauaji.
Wengine wanasema “Nilikuwa mshirika wa chama hicho kwa miaka mingi lakini sikuwahi kujua kuwa ni chama kinachomuabudu shetani” kwasababu wote tuliokuwa ndani ya chama hicho wenye degree ndogo, tulikuwa na upendo, na tulikuwa tunasaidiana, na kupeana fursa..Mpaka nilipofika ngazi za juu ndipo nilipoelewa kuwa sio sehemu salama”..mmoja aliyekuwa na degree ya 2 aliyetolewa huko na Bwana Yesu alihojiwa… je! ulishawahi kumuona shetani ndani ya ibada zenu?…akasema la! hata siku moja, wala sijawahi kuona vitu vya kiroho kama mapepo ndani ya logde! nilikuwa naingia na kutoka tu kama ninavyoingia kanisani…Na wala nilikuwa siamini kwamba ni kikundi kibaya kwa miaka kadhaa…na wala sikuwahi kutoa kafara yeyote ya mtu! mpaka baadaye sana nilipokuja kugundua kuwa hayo yanafanyika na wenye shahada za juu na hawatuambii sisi.
Kuanzia shahada ya 30 na kuendelea ndio wanaotokewa na mapepo na kuzungumza na shetani mwenyewe, na hao ndio wanaojua siri nyingi za chama hicho kuwa ni chama cha kumwabudu shetani moja kwa moja! na agenda kubwa ya chama hicho ni “kuikimbiza dunia katika ustaarabu mpya wa ulimwengu” ambao utakuja kuhasisiwa na Mpinga-kristo, chini ya utawala wa kirumi” katika siku za mwisho, lakini wengine wa shahada za chini hawaelewi sana.(www.wingulamashahidi.org)
Freemasons pamoja na vikundi vingine vya kichawi kama Iluminati, Brotherhood, ku-klax-klan,sisterhood, vinafanya kazi zinazofanana..Vyote ni vikundi vya kumwabudu shetani. Kwahiyo sio wote waliojiunga na freemasons wanaoelewa wapo sehemu gani.
Dhana iliyopo sasa hivi, ambayo hiyo inatokana na kukosa maarifa ni kwamba mtu aliyejiunga na freemasons tayari huyo ni pepo! hapana! hiyo si kweli kama tulivyotangulia kusema wapo wengine hawajui chochote wamedanganyika tu wakidhani kuwa ni kikundi cha kijamii cha kusaidiana kama vikundi vingine, hawaelewi vizuri freemason ni nini..Sasa hao wanahitaji msaada! Kumbuka ni watu kama wewe na mimi, wanapumua, wanasikia maumivu, wana hofu kama wewe na mimi, hivyo ni wa kusaidiwa kutoka huko kabla hawajazama kikabisa kabisa humo…sio wa kuwakimbia…Wanahitaji injili ya Yesu Kristo ya msamaha wa dhambi..wengine hawaelewi wamepelekwa tu na marafiki zao, ni kama tu makahaba waliojiingiza kwenye madanguro sio wote wanaelewa madhara ya kuwa kule, wanahitaji wokovu kama wewe ulioupata.
Ukienda pasipo maarifa kwa mtu ambaye ni freemason na kumwambia wewe ni shetani! unaabudu shetani na unatokewa na shetani kila siku na kuzungumza naye na kuua watu na kuwatoa kafara! na unakunywa damu…kwasababu tu umemwona kavaa pete yenye alama zao…
Ni rahisi sana kumkosa kwasababu hivyo unavyovisema unaweza kuta havifanyi katika levo aliyopo huko…kwasababu wote wanaojiunga huko kwa mara ya kwanza ni lazima wadanganywe… Hivyo huyo ni kumweleza kwa maarifa mwanzo wa chama hicho na mwisho wake.. Na kumweleza Injili ya Yesu Kristo ya msalaba…Lakini ukikutana naye na kuanza tu! kukemea hapo hapo! na kumwogopa!…na kumhakikishia kwamba yeye ni mchawi..atakushangaa sana na hatakuelewa, na pengine atakuchukia na itamfanya azidi kuamini kuwa yupo sehemu salama zaidi. Wengi waliojiunga huko ni kwasababu wamekosa maarifa..Hivyo wanatakiwa waokolewa kwa kupewa maarifa ya Neno la Mungu. Hivyo usikose maarifa ya namna ya kuvua roho za watu!.
Biblia inasema katika
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..”
Na pia jambo lingine watu wasilolijua ni kwamba Freemasons watu hawajiungi kwa kupitia Facebook, wala hawajiungi kwa kupitia vipeperushi huko barabarani, wala vinakala juu ya nguzo za umeme…Huo wote ni utapeli tu ambao watu wanadanganywa…Ni watu wa kawaida ambao wanatafuta kupata pesa za kitapeli. Na pia freemasons ni kitu kidogo sana kwa mtu aliyeokoka haipaswi kukuzwa kiasi hicho mpaka kutengeneza hofu ya kupita pembezoni mwa barabara yenye jengo la freemasons, wala kumsalimia mtu aliyejiunga huko..Hakuna chochote kitakachokupata ukiwa ndani ya Kristo kwasababu shetani ni yule yule, unayeshindana naye kanisani ndio huyo huyo huko freemason! Sasa unachoogopa ni nini? (www.wingulamashahidi.org)
Na pia usikose maarifa kuwa freemasons ni mahali watu wanakwenda kupewa pesa!! hawaendi kupewa pesa, waliotoka huko na kumpa Bwana Maisha yao, wanasema “watu wote wanaojiunga huko ni wafanya kazi” na kule hawapewi pesa kana kwamba kuna ATM inayomwaga pesa…hapana! isipokuwa waliopo kule wanapeana fursa wao kwa wao, na ndio moja ya viapo vyao… freemasons wenzao waliopo ngazi za juu katika shughuli za ulimwengu kila mmoja ana jukumu la kumwangalia mwenzake aliye chini..
Kama mmoja yupo ngazi ya juu katika serikali anamnyanyua freemasons mwenzake aliye chini, kama mmoja ni mkurugenzi basi ikitokea nafasi ya kazi anamtafuta freemason mwenzake anamchomeka hapo n.k hiyo ndio maana unaona mtu aliyejiunga anaweza kupata maendeleo ya ghafla, na endapo akijitoa wananyang’anya ile nafasi, ndio maana unaona mtu anaporomoka ghafla. Lakini sio kwamba wanapewa hela za kimajini ambazo zinatokea tu kichawi! Huko ni kukosa maarifa!
Hivyo kama umejiunga huko! Kumbuka kujiunga kunakozungumziwa sio kwa kupitia facebook! Au mtandaoni….Kuna watu nimekutana nao, wanakuja kuomba msaada, wamedanganywa na matapeli facebook na kuambiwa wasipotuma kiasi fulani watakufa! Na hivyo wanaogopa na kutuma pesa! Hao ni matapeli..kujiunga kunakozungumziwa ni kule kuwasili kwenye hayo maukumbi yao, na kupewa viapo na kukutana na washirika wengine. Kama umejiunga kwa namna hiyo, mlango wa kutoka upo wazi.(www.wingulamashahidi.org)
Huko ulipo upo kwenye elimu ya shetani kamili, na nguvu za giza zimekufunika..Unamwabudu shetani sasa bila kujua, lakini ipo siku utamwabudu waziwazi, hivyo unayo nafasi ya kutoka…haijalishi uliapa kiasi gani! Kuwa utakitumikia chama hicho na endapo ukitaka kutoka utakufa! Nataka nikuambie hutakufa! Zaidi ya yote ukiendelea kukaa huko ndio utakufa.
Hapo ulipo fanya jambo moja la kiimani! Tubu! Na uwaambie mimi sio mmoja wenu tena! Watakutishia lakini hakuna kitakachokupata! Kwasababu aliye upande wako ni mkuu kuliko aliye upande wao. Na usiende tena huko, wala usifanye ibada zao, wala ishara zao, choma vito vyao, uniform zao, pamoja na mihamala yao..futa na namba za washirika wenzako. Tafuta kanisa la kiroho linaloamini injili kamili ya YESU KRISTO, dumu huko, Na ukae katika mafundisho ya Kweli ya Kristo Yesu. Au wasiliana nasi kupitia boxi la maoni hapo chini.
Kumbuka washirika wote wa Freemasons watakwenda kuzimu kwasababu wanamwabudu shetani kama wasipotubu! Hivyo kama hutatubu utakwenda kuzimu….Hivyo kwa hitimisho freemason ni nini?…jibu ni kikundi cha kishetani kinachomwabudu shetani.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/14/freemasons-ni-nini-na-mtu-atatokaje-huko/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.