KAFIRI NI NANI KULINGANA NA BIBLIA?

by Admin | 19 October 2019 08:46 pm10

KAFIRI NI NANI?

Kafiri ni Mtu yeyote asiyeamini IMANI fulani…kafiri Katika Biblia ni mtu yeyote asiyeuamini Ukristo, Ukafiri hauna tofauti sana na upagani, Mtu yeyote asiyemwamini Bwana Yesu Kristo kwamba alikuja, na kufa kwaajili ya dhambi za ulimwengu mtu huyo ni kafiri.

Mtu yeyote asiyeshika njia za Bwana Yesu Kristo na kumkana  mtu huyo  kafiri.

Yuda 1:14 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo”

Kwahiyo kafiri ni nani?…Jibu: Ni mtu yeyote asiyempenda Bwana YESU huyo ni kafiri, na tena Biblia inasema Amelaaniwa

2Wakorintho 16:22 “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha”.

Kwahiyo mtu yeyote akitaka asiwe kafiri, ni sharti amkiri Yesu Kristo, na kumwamini, na kumpa Maisha yake na kudhamiria kuacha dhambi.

Na makafiri wote hawataurithi uzima wa milele. kwasababu hawajamwamini Mwana pekee wa Mungu (Yesu Kristo)

Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.

Ubarikiwe sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MPAGANI NI NANI?

WAPUNGA PEPO NI WATU WA NAMNA GANI?

NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

JE! MTU KUSIKIA SAUTI ZA WATU WALIO MBALI, KUNAWEZA TOKANA NA MUNGU?

NA MTU MMOJA AKAVUTA UPINDE KWA KUBAHATISHA, AKAMPIGA MFALME

Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/19/kafiri-ni-nani/