WACHAWI

by Admin | 29 November 2019 08:46 pm11

Je! Wachawi wapo?..Wachawi wanaua watu?, wachawi ni wengi?, Nitajikingaje na wachawi?.Je wachawi wanapaa kwa ungo?

Kuna maswali mengi sana yahusuyo wachawi..Lakini kabla ya kuyajibu maswali hayo hapo juu..Ni vema tukajua nini maana ya uchawi..Kwa kujua nini maana ya uchawi unaweza kubofya hapa usome kisha ndipo tuende pamoja. >> Nini maana ya uchawi

Je wachawi wapo?

Kwa ufupi uchawi upo.  Biblia Takatifu inathibitisha hilo.Ni kitu kinachoogopeka sana na wengi wasio na Maarifa ya kutosha yamhusuyo Mungu. Na kama uchawi upo maana yake na wachawi wapo pia. Kwasababu wanauoufanya huo uchawi ndio wanaoitwa Wachawi.

Biblia inawataja wachawi katika..

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako”.

Na katika kitabu cha Matendo tunamsoma mtu mmoja aliyekuwa mchawi.

Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;”

Kwahiyo wachawi wapo 

Je Wachawi wanaua watu?

Jibu ni ndio!..Wachawi wanaua watu na wanauwezo wa kumdhuru mtu yeyote aliye nje ya Kristo. Kwasababu mtu yeyote aliye nje ya Kristo hana ulinzi wowote wa KiMungu hivyo chochote kile kinauwezo wa kumdhuru..Na wachawi wanauwezo wa kumdhuru mtu kwa uchawi.

Je Wachawi ni wengi?

Ipo idadi kubwa ya wachawi ulimwenguni kote..Kikundi kimoja cha Freemason ambacho ni cha kichawi, kina washirika zaidi ya milioni 6 duniani kote. Na kuna maelfu ya vikundi hivyo katika kila nchi duniani kote. Hivyo kwa ufupi wachawi ni wengi.

Je wachawi wanapaa kwa ungo?

Kama vile maarifa ya wanadamu yalivyo na aina mbalimbali ya vyombo vya usafiri, kwamfano kuna magari, ndege, pikipiki, baiskeli n.k Vivyo hivyo elimu ya uchawi. Wapo wanaotumia ungo kusafiria, wapo wanaotumia ufagio, wapo wanaotumia fimbo, wanyama n.k

Lakini Elimu ya Uchawi ni dhaifu sana…Kiasi kwamba haistahili kulinganishwa na Elimu ya Mungu hata kidogo. Elimu ya Mungu ni kuu sana

Je wachawi ni wa kuogopwa?

Mchawi yoyote hawezi kumwingilia Mtu aliyeokoka…Kwanini? Kwasababu Elimu ya Mungu ni kuu sana..Mchawi ajaribupo kumwigia mtu aliyeokoka..Anaweza akakutana na moja ya mambo yafuatayo.

  1. Anaweza kuona chochote kisicho cha kawaida kikimzunguka yule mtu wa Mungu, inaweza ikawa moto, au mwanga mkali, au anaweza asimwone kabisa.
  2. Anaweza akaona Malaika..Wachawi wengi wanakutana na Malaika wakiwalinda watu wa Mungu, na wengi wa wachawi wanaoona hivyo huwa hawatangazi inaishia kuwa siri yao…Labda wakiokoka ndio wanaweza kutoa ushuhuda…

Je tutashindanaje na wachawi?

Tofauti na inavyodhaniwa na wengi kwamba wachawi tutawashinda tu kwa kuwatupia mishale ya moto katika maombi ya vita vikali vya mkesha…Lakini ukweli ni kwamba mtu tu aliyesimama katika Imani kamilifu,aliyemwaminifu kwa Bwana katika utakatifu na utauwa..Hata asipoomba ombi lolote katika maisha yake linalomhusisha mchawi…bado mtu huyo atakuwa yu salama dhidi ya wachawi.

Mungu hatulindi kwasababu tunawajua maadui zetu..Ndugu ukifunuliwa macho idadi ya maadui ulionao katika ulimwengu wa roho, na ukaambiwa uanze mmoja mmoja kupambana naye… utapambana vita milele na milele na bado hutamaliza hata robo yao..

Wakati wewe unawataja wachawi wako watano hapo mtaani wanakuzunguka…Nyuma ya pazia kuna jeshi la mapepo yanakuwinda usiku na mchana..Kuna pepo ambalo usiku na mchana linapambana tu ujikwae chooni uanguke ufe…Lipo ambalo shughuli yake ni kutafuta kila namna ya wewe kugongwa na gari kila unapotoka nje…lingine ufe na ajali..Pepo lingine ni ili ung’atwe hata na nyoka tu au mbwa mwenye kichaa barabarani…Usiku na mchana yanakufuatilia kila unapotoka, unapokwenda na Mungu anakuepushia nayo. Pasipo hata wewe kujua.

Kwahiyo kamwe usifikiri maombi yako ya vita ndiyo yanayokusaidia sana katika kukulinda..Wachawi ni moja ya maadui wadogo sana wa uzima wako.

Kitu kikubwa kinachokusaidia kukulinda ni wewe kukaa katika maisha yanayompendeza Mungu basii, kuzishika amri zake na kudumu katika Neno lake. Hata usipowataja hao wachawi katika maombi yako kwa miaka 10 hakuna watakalofanya litakalofanikiwa juu yako…Mapepo na wachawi kila watakachokipanga hakitafanikiwa..Uthibitisho utaona tu ni wewe upo salama..Kwasababu Mungu wetu anatupigania kwa namna isiyoonekana.

Je tunapaswa kuogopa kula nyumbani kwa mchawi?

Hatupaswi kuogopa kula chochote kilichopo mbele yetu, kwa hofu ya kulogwa, wala hatupaswi kuogopa kusafiri mkoa wowote au nchi yoyote kwa hofu ya kulogwa. Wala hatupaswi kuogopa kuwapa kuwashika mkono watu ambao tumeshajua ni wachawi au waganga wa kienyeji… Kwasababu tunaye Kristo ambaye anatupigania kwa namna isiyoonekana. 

Je tunapogundua fulani anajihusisha na Uchawi tumfanyeje?

Hatupaswi kumtenga wala kumuua?..wala kumchukia…Kwasababu Uchawi ni dhambi kama dhambi nyingine..Na dawa ya dhambi ni Toba, itokanayo na Injili ya Msalaba…Hivyo mtu yeyote ambaye ni mchawi anaweza tu kuacha uchawi kwa kuhubiriwa injili..ambayo hiyo ni silaha tosha kuifanya kila fikra iweze kumtii Kristo. Na baada yakuhubiriwa Roho Mtakatifu atamchoma ndani yake na kugundua alikuwa gizani na hivyo kuokoka na kuwa kiumbe kipya na kuifanya kazi ya Mungu. Hiyo ndiyo silaha ya kumvua mchawi uchawi wake..Na sio kumkemea wala kumuua.

2 Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;

4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;”

Ikiwa hujaokoka!. Ni vyema ukafanya hivyo leo…Hakuna ulinzi wowote mtu anaweza kuupata akiwa nje ya Kristo..Mtu aliye nje ya Kristo kamwe hatawaweza wachawi, wala hataweza kushindana na roho ya uadui inayotenda kazi ndani ya mapepo wabaya…

Hivyo Kristo pekee ndiye anayetoa utakatifu..Mpokee leo na kisha Ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa waji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi na utakuwa umezaliwa mara ya pili kwa Roho atakayeingia ndani yako. Na hapo utakuwa chini ya mikono salama ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUTOKA NJE YA MWILI WAKE?.

https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/maswali-na-majibu-2/

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/11/29/wachawi/