BIRIKA LA SILOAMU.

by Admin | 12 December 2019 08:46 pm12

BIRIKA LA SILOAMU…Bwana Yesu alisema..”Mtu akiona kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Shalom, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu ambalo ni mwanga wa njia zetu, na taa iongozayo miguu yetu.

Yohana 9:6 “Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho,

7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona”

Bwana wetu Yesu angeweza kumponya mtu huyu pasipo hata kumwambia akanawe katika birika la Siloamu.. Tafsiri ya birika ilivyotumika hapo sio birika la kuwekea chai au maji ya moto..hapana! bali birika maana yake ni Bwawa dogo lililotengenezwa kwa kusudi maalumu…ni kama swimming pool kwa lugha ya kiingereza..

Katika Yerusalemu zamani za agano la kale, lilikuwepo birika hilo ambalo lilitengenezwa mara ya kwanza na Mfalme wa Israeli aliyeitwa Hezekia, ukisoma 2Wafalme 20:20 utaliona jambo hilo,..lakini birika hilo lilikuja kubomolewa na Mfalme wa Babeli Nebukadneza, lakini baadaye lilikuja kutengenezwa tena na Nehemia…na likaendelea kuwepo mpaka wakati wa kipindi cha Bwana Yesu…ingawa lilikuja kufanyiwa ukarabati tena na Herode.

Biblia inasema.

Yohana 7: 37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”.

Utaona mahali pengine pia Bwana Yesu alitumia mfano wa maji ya kisimani kufundisha juu ya maji ya rohoni..

Yohana 4: 6 “Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.

7 Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.

8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula.

9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria).

10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.

11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?

12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?

13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.

16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa”

Je umeyapata hayo maji?..Roho Mtakatifu ndiye maji ya Uzima..anakata kiu ya dhambi, kiu ya uasherati, kiu ya rushwa,kiu ya wizi na kila aina ya uchafu, maji hayo yanapatikana bure…

Bwana Yesu alisema mwenye hivyo…

Ufunuo 21: 6 “Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure”

Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Pengine umesikia habari hizi za maji ya uzima mara nyingi sana zisizohesabika…lakini nataka nikuambie ukiyadharau haya maji leo yanayopatikana bure utayatamani siku ile katika ziwa la moto na utayakosa kama yule Tajiri aliyemwomba Lazaro achovye kidole chake kwenye maji hayo ili auburudishe ulimi wake akakosa…Na ndivyo siku ile utayatamani maji hayo utayakosa…usikazane kutafuta maji ya upako, au kutafuta kuzamishwa kwenye mabwawa yajulikanayo kama mabwawa ya upako..tafuta MAJI YA UZIMA…Bwana atusaidie tuyapate maji haya kwa wingi..ili tuwe na Uzima…Tunamshukuru sana Bwana wetu Yesu Kristo wa kutuletea maji haya ya uzima..jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

UMEPATANISHWA NA MAADUI ZAKO?

KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.

KIJITO CHA UTAKASO.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/12/12/birika-la-siloamu/