BWANA HUWAJUA HAO WAMKIMBILIAO.

by Admin | 26 February 2020 08:46 pm02

Nahumu 1:7 “Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao”.

Nataka nikuambie wewe uliyemfanya Mungu kuwa sehemu yote ya Maisha yako bila unafki, ujue kuwa Mungu anakuona, wewe ambaye umemfanya kuwa tegemeo lako la mwisho, Mungu anakuona, wewe ambaye muda wote unatenga kumuwaza yeye, kuzifikiria habari zake, unajishughulisha kuifanya kazi yake, bila kuangalia mazingira uliyopo, wewe ambaye unajibidiisha kutafuta maarifa yake bila kuchoka, japo wengine watakuona kama umerukwa na akili au unapoteza muda…Ujue Mungu anakujua vyema sana.

Haijalishi ulimwengu utakuona umepotea kiasi gani, au ndugu wamekukataa vipi, au marafiki wamejitenga nawe mbali kiasi gani…Hilo halimfanya Mungu asikuone.. Anakuona sana, kuliko hata wewe unavyodhani..

Nyakati hizi za mwisho. Ni rahisi kuona hata mlevi, au mzinzi, au mvaaji vimini anasema Mungu ndiye kimbilio langu,..ni mshirika mzuri wa kanisani anaimba kwaya, au ni kiongozi wa vijana, au wa wakina mama, lakini ni mtazamaji pornography na mzinzi naye pia anasema Mungu ndiye kimbilio langu..kila mtu atasema hivyo maadamu ni rahisi tu kulitamka hilo neno..Lakini Mungu anasema..mimi nawajua wanikimbiliao.

Haihitaji kukaa chini na kumsimulia, au kumweleza katika maombi, au kumwimbia nyimbo nzuri na kumwambia wewe Mungu ni kimbilio langu, au kumueleza kila mtu jambo hilo..hilo halikupi tiketi ya Mungu kukuona kuwa umemkimbilia..Bali matendo yako kwake yatazungumza, Kwake hakuna siasa..

Lakini nataka nikuambie ipo faida kubwa sana, na thawabu kubwa uliyowekewa wewe unayemtafuta Mungu kwa nguvu zako zote..Ipo siku ukiwa hapa hapa duniani utaburudishwa sana, kabla hata ya kwenda mbinguni kama usipozimia moyo..

Zaburi 31: 19 “Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!

20 Utawasitiri na fitina za watu Katika sitara ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na mashindano ya ndimi”.

Hivyo usikate tamaa. Yeye siku zote huwajua hao wamkimbiliao

Mungu akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Mpagani ni nani?

EWE MKE! HESHIMA YAKO IPO KWA WAKWE ZAKO.

MPINGA-KRISTO

JIWE LA KUKWAZA

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/26/bwana-huwajua-hao-wamkimbiliao/