Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?

by Admin | 12 March 2020 08:46 pm03

SWALI: Naomba kufahamu,Yale maneno yanayookana juu ya msalaba wa Bwana Yesu (I.N.R.I) yana maana gani, Nimekuwa nikiyaona kwenye picha za msalaba lakini siyaoni mahali popote kwenye biblia?.


JIBU: Tukisoma kitabu cha Yohana sura ya 19 mstari wa 19-20 inasema..

 “Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.

20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani”.

Kama tunavyosoma,. Pale juu  ya msalaba wa Bwana Yesu, Pilato alingongelea kibao ambacho kilikuwa kinamwelezea kuwa yeye ni nani,.. Sasa maneno hayo YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI  kwa Kilatino (au, Kirumi) yanasomeka hivi…”Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum.” Na kifupi chake ndio hiyo  I.N.R.I…

Sasa madhehebu mengi hususani, Katoliki, Anglikana na Lutheran, wanapenda kutumia  Ufipisho huo wa lugha ya kilatino (kirumi), kiyawakilisha yale maneno yaliyoandikwa juu ya msalaba wa Yesu.

Lakini Ukweli ni kwamba juu ya msalaba, hayakuandikwa maneno yale katika ufupisho wowote, bali yaliandikwa vile vile kama  yalivyokuwa tena  kwa lugha zote tatu, ili kila mtu aliyepita aweze kuyasoma, na ndio maana wale Mafarisayo wakamwambia Pilato. Usiandike, kuwa huyu ni Mfalme wa Wayahudi; bali andika kuwa  yeye ndio anajiita, mfalme wa Wayahudi…Unaona ikiashiria kwamba maandishi yale yalikuwa yanasomeka kabisa na sio kwamba yameandikwa kwa kifupisho fulani.

Lakini pamoja na hayo yote, kujua au kutokuja msalaba ulikuwaje, kwamba ulikuwa ni mrefu sana, au ni mfupi sana, au ulikuwa ni wa alama ya kujumlisha, au ni wa nguzo iliyosimama, au kwamba maandishi yake yaliandikwa kwa wino wa bluu au wa njano, Hayo yote hayachangii chochote katika wokovu wetu?? Kwasababu hata katika Neno hilo hilo YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI, ukisoma injili nyingine utaona linasema  tu MFALME WA WAYAHUDI(Marko 15:26), na sehemu nyingine linasema  HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI(Luka 23:38)..Unaona sasa ukiyatafsiri hayo katika lugha ya kilatino (kirumi) utaona ni tofauti kabisa na hiyo  yenye kifupisho cha INRI.

Sasa Hiyo yote ni kutufundisha kuwa tunachopaswa kujua ni kwamba Kristo alisulibiwa juu ya mti, na kwamba kusulibiwa kwake kumeleta ondoleo la dhambi la maisha yetu. Hicho ndicho kiini cha msalaba, na kwamba yoyote amwaminiye Yesu Kristo atapata ondoleo la dhambi zake na ukombozi wa Maisha yake,  Hivyo tusiitazame misalaba sana, na kuipa heshima mpaka sasa imeshawafanya wengine wafikie hatua ya kuiabudu na kuisujudia..jambo ambalo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.

Ubarikiwe.

Tafadhali share na wengine.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

Yeremia 33:3 (NIITE NAMI NITAKUITIKIA)

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

KWANINI NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/03/12/neno-i-n-r-i-kwenye-msalaba-wa-bwana-yesu-maana-yake-ni-nini/