Yeremia 33:3 (NIITE NAMI NITAKUITIKIA)

Yeremia 33:3 (NIITE NAMI NITAKUITIKIA)

Katika kitabu cha Yeremia 33:3 biblia inasema maneno haya…..”Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”.

Maneno haya ni Mungu aliyazungumza kwa kinywa cha Yeremia, alipokuwa katika gereza alilokuwa amefungwa, wakati huo Mji wa Yerusalemu ulikuwa umeshazungukwa na majeshi ya Nebukadneza, na ndani ya mji kuna njaa kali. Na tayari Bwana alikuwa ameshawaambia penda wasipende watakwenda Babeli tu..utumwani kutokana na maovu yao yasiyokuwa na toba, japokuwa wameonywa miaka mingi watubu lakini wamekataa.

Lakini kama biblia inavyosema “Mungu hatamtupa mtu hata milele (Maombolezo 3:31)”. Maana yake ni kwamba kutakapotokea mitikisiko hata mtu akageuka na kumwacha Mungu na mtu yule akaadhibiwa katika dhambi zake, na mtu yule akatubu mbele za Mungu…Basi Mungu hataishikilia adhabu yake juu ya huyo mtu milele..Itafika kipindi atamrehemu tu…ooh ni Mzuri kiasi gani huyu Mungu wetu?.

Sasa katikati ya kipindi hicho cha kujeruhiwa na Bwana, katikati ya kipindi hicho cha kuumizwa na Bwana kutokana na makosa uliyoyafanya..katikati ya kipindi hicho Bwana alichokuadhibu baada ya kuonywa mara nyingi juu ya uasherati wako, juu ya wizi wako, juu ya ujambazi wako, juu ya ubaya wako wote..upo kipindi unaitumikia Adhabu ya Mungu wako kwa makosa uliyoyafanya..kipindi ambacho maji yapo shingoni..

Kipindi hicho ndicho anachomwambia Nabii Yeremia kwamba awaambie watu wake..wafikiapo kipindi kama hicho “wamwite Mungu naye atawaitikia”.

Upo taabuni kwa sababu ya dhambi zako..Tubu leo kwa kumaanisha na kiri kuwa umekosa…na wala usione umeonewa wala usijihesabie haki..kubali umestahili adhabu hiyo, kutokana na makosa yako..na Bwana amekuzuia kila kona kila pembe, unaona mauti tu..

Zaburi 107:10 “Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na chuma,

11 Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, Wakalidharau shauri lake Aliye juu.

12 Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.

13 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao”

Baada ya kutubu..Leo hii hili ni Neno lako.

Yeremia 33:3 “Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”.

Japokuwa umemwasi Bwana kama wana wa Israeli lakini bado lipo tumaini la kuonyeshwa MAMBO MAKUBWA. Japo kuwa unaona umeshakwisha na kupotea kabisa lakini Bwana atakuonyesha MAMBO MAGUMU pia usiyoyajua.

Lakini anachokihitaji kutoka kwako na kwangu..Ni toba kamili kutoka moyoni..Ndio maana amekushusha hivyo lakini yeye moyoni mwake hapendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha kama alivyosema mwenyewe katika Maombolezo 3:33.

Bwana akubariki

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

USHAURI KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.

MKUU WA ANGA.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 7 (Yeremia na Maombolezo)

TIMAZI NI NINI

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

2 comments so far

Maiko beddaPosted on3:16 um - Septemba 23, 2021

Mungu awabariki,hakika ni neno la matmaini.

Leave a Reply