Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?

by Admin | 8 April 2020 08:46 pm04

Je! ni kweli Bwana Yesu alibatiza mtu akiwa hapa duniani?


JIBU: Bwana Yesu yeye mwenyewe hakubatiza bali wanafunzi wake ndio waliobatiza kwa agizo lake yeye. Hata leo mkuu wa nchi akitoa agizo la ujenzi wa jengo Fulani la serikali…Jengo lile litakapojengwa na kumalizika..jengo hilo litajulikana kama limejengwa na Mkuu huyo…lakini kiuhalisia sio yeye aliyelijenga waliolijenga ni wale vibarua na wafanyakazi wake…lakini kwasababu ni mkuu ndio katoa hiyo amri na fedha basi ni sahihi kabisa kusema ni Mkuu huyo ndiye kajenga jengo lile.

Kadhalika kuna mahali kwenye biblia paliposema Bwana Yesu alibatiza…lakini ukiendelea mbele kidogo utaona biblia imefafanua zaidi waliobatiza ni wakina nani…kwamba ni wanafunzi wake kwa amri yake na sio Bwana Yesu mwenyewe.

Tusome.

Yohana 4:1 “Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza,

2 (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,)

3 aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya”.

Unaona hapo mstari wa pili unafafanua zaidi kwamba siye Bwana Yesu aliyebatiza bali ni wanafunzi wake.

Pamoja na hayo yote Jambo lingine la msingi hapo la kujifunza ni kwamba watu walianza kubatizwa kabla hata ya Bwana Yesu kusulubiwa, kufa na kufufuka ..kuonyesha ni jingi gani ubatizo ulivyokuwa wa muhimu…Ni agizo la awali kabisa pale mtu anapomwamini Yesu na kutubu dhambi zake.

Hivyo nasi tunajifunza kama hatujazingatia kwenda kubatizwa ubatizo sahihi tukidhani sio agizo la msingi, hapa tunaonyeshwa watu walianza kubatizwa kabla ya Kristo kwenda Golgotha, ..kuashiria umuhimu wa hicho kitu, na kumbuka pia ubatizo hautekelezwi kama mtu anavyoamua kwamba unaweza kuzamishwa kichwa tu kwenye maji na ukawa tayari umeshabatizwa, au unaweza kutumia mchanga badala ya maji, au unaweza kunyunyiziwa tu badala ya kuzama mwili mzima…hakuna njia mbadala ya ubatizo..Neno ubatizo maana yake ni KUZAMISHWA. Na kuzama maana yake ni kuzama hakuna maana nyingine ya neno hilo. Hivyo tunazamishwa katika maji mengi (kama Yohana 3:23 inavyosema), na kwa Jina la Bwana Yesu Kristo kama (Matendo 2:38,8:16, 10:48, 19:5 inavyosema).

Tuyazingatie hayo na Bwana atatukubali na kutubariki.

Shalom.

Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=68fHuz_icug[/embedyt]

Mada Nyinginezo:

MIILI YA UTUKUFU ITAKUWAJE?

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

LIVUNJENI HEKALU HILI, NAMI KATIKA SIKU TATU NITALISIMAMISHA.

MWACHE YESU, NDIO AWE WA  KWANZA KUKUHURUMIA.

LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI.

RABI, UNAKAA WAPI?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/04/08/je-bwana-yesu-alibatiza-akiwa-hapa-duniani/