NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?

by Admin | 21 April 2020 08:46 pm04

Shalom karibu tujifunze Biblia, kwasababu Neno la Mungu ndio mwanga wa njia zetu na taa iongozayo miguu yetu.

Ni wapi mahali sahihi pa kulipa zaka je ni kanisani, au kwa mayatima au kwa wajane?..Hili ni swali linaloulizwa na wengi..Leo kwa neema za Bwana tutajifunza..

Andiko linalofahamika na wengi wetu lihusulo mahali sahihi pa kulipa zaka ni hili..

Kumbukumbu 26:12 “Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;”  

Sasa kabla ya kuingia kwa undani kulielezea andiko hili..ni muhimu kwanza kufahamu mambo machache yafuatayo..

Kwa mtu aliyeokoka na kuitambua Neema ya Yesu kikweli kweli, Zaka ni jambo la lazima ingawa sio la sheria.(Mathayo 23:23)

Ipo michango mingine tofauti na Zaka..ambayo ni ya muhimu pia kwa kila aliyebadilishwa na kuwa mkristo kuitoa…na michango hiyo ni CHANGIZO, na SADAKA…Hii miwili ni tofauti na Zaka…Zaka ni sehemu ya Kumi ya Mapato…Changizo ni chochote ambacho mtu anaweza kumtolea Mungu kama mchango, (hakina sheria, wala kiwango maalumu)..na sadaka ni dhabihu mtu anayomtolea Mungu wake, inaweza kuwa sadaka ya shukrani, ya malimbuko, au ya ombi ya kutimiziwa hitaji fulani.(Warumi 15:26, 1Wakorintho 16:1 )

Jambo la tatu la kufahamu ni kwamba..Zaka/fungu la 10…Ndiyo sadaka inayopaswa ichukuliwe kuwa ya kiwango cha chini kuliko hizo nyingine zote… haipaswi kuchukuliwa kama ni adhabu wala kitu kikubwa kuliko vingine…(maana yake changizo na sadaka zinaweza kuzidi mara nyingi sana Zaidi ya zaka).

Sasa tukirudi kwenye swali letu..Je! zaka inapaswa itolewe wapi..JIBU NI RAHISI INAPASWA ITOLEWE KANISANI TU!!…Na si penginepo!..Michango mingine inaweza kwenda kwa masikini, kwa wasio jiweza ambayo hiyo inaweza ikawa hata ni nyingi sana kuliko zaka..Kwa mfano mtu aliyepata mapato ya laki moja, maana yake hapo zaka ni elfu 10..kilichosalia ana uhuru nacho kusaidia kiwango chochote kwa wasiojiweza na masikini wa mitaani, kama atawapa elfu 50 au Zaidi ya hapo ni mapenzi yake mwenyewe..na tena ni vizuri Zaidi…Kwasababu ndivyo atakavyojiwekea daraja zuri Zaidi la kubarikiwa kama maandiko yanavyosema heri kutoa kuliko kupokea, lakini ZAKA ni kanisani tu!.

Sasa swali linakuja..kwanini hapo juu kwenye Kumbukumbu la Torati, maandiko yanasema zaka iliwe na maskini, mjane, yatima na Mlawi?.

Jibu rahisi ni kwamba katika Agano la kale…Kanisa la Mungu lilikuwa ni jamii nzima ya wana wa Israeli…Wote waliovuka bahari ya shamu hilo ndilo lililokuwa kanisa la kwanza yaani uzao wa Ibrahimu…Hivyo Zaka zililihusu kanisa hilo lote kwa ujumla…ambapo ilikuwa inawekwa kwa utaratibu maalumu kwamba walio wajane kweli kweli ambao hawana watu wa kuwasaidia, Pamoja na walawi(yaani makuhani na uzao wao) ambao hawa hawakuwa na shughuli yoyote Zaidi ya kuhudumu katika nyumba ya Mungu…pamoja na mayatima wasio na ndugu wala wazazi na wageni walio wayahudi..Kwa utaratibu maalumu Zaka waligawanyiwa wao.

Hivyo kwa ujumla hilo ndilo lililokuwa kanisa la Mungu la kwanza…Utauliza ni wapi wana wa Israeli walijulikana kama ni kanisa…Soma, Matendo 7:37-38. Hivyo zaka ziliwahusu wana wa Israeli tu.. yaani maskini, walawi, wajane, na mayatima na wa Israeli tu..hazikuwahusu maskini waliokuwepo Babeli, wala wajane wa Ashuru.

Na katika Agano jipya…Zaka zinalihusu kanisa la Kristo peke yake…na si penginepo…Yaani maana yake ni kwamba (wajane,yatima, maskini, na walawi ambao kwasasa wanawakilisha wachungaji, waalimu,manabii, mitume na wote wanaohudumu madhahabuni, au wanaoifanya kazi ya Mungu kwa ujumla wake)..Hao ndio wanaopaswa kunufaika na zaka zitolewazo…na si wajane wa mitaani, au maskini tunaopishana nao barabarani…hao wanaweza kupewa michango ambayo mtu anaweza kutoa kama apendavyo..na pia inaweza ikazidi hata kiwango cha zaka..sio dhambi….lakini zaka ni kwa KANISA TU!. Maana yake kwa wajane ambao ni wakristo waliopo pale kanisani ambao ni wajane kweli kweli, wamedumu katika utakatifu na kuosha watakatifu miguu kama maandiko yanavyosema katika…1Timotheo 5:9-16,..Na mayatima ni hivyo hivyo…wale ambao ni wakristo au wazazi wao walikuwa ni wakristo walioshuhudiwa na kanisa.

Sasa swali linakuja..je nikipata zaka nimtafute Yatima fulani au mjane fulani pale kanisani nimpe, au nimtafute mchungaji pale kanisani au nabii nimpe kwa siri, nitakuwa tayari nimeshalipa Zaka??…Jibu ni hapana!..hupaswi kwenda kumpa mchungaji binafsi zaka yako, wala yatima binafsi, wala mjane..Kama unataka kufanya hivyo basi unaweza kufanya kama mchango tu kwao, yaani ukawatafuta wao binafsi kwa fedha yako ukawapa lakini zaka usifanye hivyo…

Tayari tumeshapewa utaratibu katika biblia wa namna ya kulipa zaka..

Tusome…

Matendo 4: 32 “ Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 

33  Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. 

34  Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, 

35  wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji”.

Umeona hapo?..wote walipeleka sadaka zao na zaka zao miguuni mwa mitume…Na ndipo Mitume wakawa wanawagawia kila mtu kama alivyohitaji (maana yake kila mkristo mwenye mahitaji, na sio maskini wa barabarani), Hivyo wenye mahitaji walikuwa wanachunguzwa kwanza wenye vigezo vya kimaandiko vya kupewa ndipo wanapewa sio tu kila mtu ambaye anashida anapewa tu hapana!..palikuwa na utaratibu…Na kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utakuja kuona kuwa hata bado huo mfumo ulikuwa ni ngumu kuusimamia mitume..mpaka wakaweka watu wengine 7 wenye hekima Zaidi, ambao wataweza kujua na kusimamia ni nani anastahili Zaidi na nani hastahili, na ni nani anapaswa apate Zaidi na nani asipate, Ndio wakapatikana wakina Stefano huko huko ambao ndio walikuwa mashemasi…Sasa Mashemasi kazi yao ndio hiyo kusimamia bajeti ya kanisa na kuigawanya kwa watu kulingana na katiba ya kimaandiko.

Kwahiyo kwa hitimisho katika Agano la kale na agano jipya…hakuna mahali popote zaka walipelekewa watu wa nje ya kanisa…na kulikuwa na utaratibu maalumu. Hivyo kama kuna mtu umemwona ana uhitaji labda umekutana naye barabarani, au mtaani au popote pale nje ya kanisa mpe kwa kadiri uwezavyo lakini si zaka..zaka yako peleka katika kanisa lako unaloshiriki(hiyo inawahusu watakatifu)…Huko kama ni kanisa la kweli la Kristo wanaujua utaratibu wa kimaandiko wa namna ya kuigawanya.

Bwana akubariki..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UFANYE NINI KAMA MKRISTO WAKATI HUU WA JANGA LA CORONA?

UFUNUO:Mlango wa 6-( Maelezo ya Muhuri saba)

JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.

NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;

Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/04/21/ni-wapi-mahali-sahihi-pa-kulipa-zaka/