Je Mtu anaweza kusema uongo, Na Mungu akambariki?

by Admin | 23 April 2020 08:46 pm04

SWALI: Shalom, naomba msaada wenu kuna sehemu zimenichanganya.. Kutoka 1:15-20 ..wale wazalishaji wa kimisri.. wanatumia uongo na Mungu anawabariki… swali langu .. Je busara ya uongo inaweza tumika na isiwe kikwazo mbele ya mtu wa Mungu…


JIBU: Kama ulivyosema busara ya uongo..maana yake kuna uongo wa busara na usio wa busara…Wenye busara ni ule wenye nia ya kujenga na usio wa busara ni ule wenye nia ya kuharibu ambao ni wa Adui shetani.

Tuchukue mfano…mtoto mdogo wa miaka 5 anakuuliza mama/Baba eti Watoto wachanga wanatokea wapi?…sasa si busara kumweleze hatua zote za mtoto kuzaliwa..kwamba kuna vitendo vya kama kukutana kimwili vinahusika…kwa umri wake ule hastahili kufahamu hayo mambo..kwahiyo utamwambia tu kama tulivyokuwa tunaambiwa sisi tulivyokuwa wadogo kwamba “wanapatikana kwenye maua mazuri tu”..Huo ni uongo wa busara…na si dhambi.

Hali kadhalika ndugu yako amekuja kuomba msaada kwako na akakueleza siri zake za ndani sana na amekuomba tafadhali sana usimwambie mtu…na baada ya kutoka hapo..baadhi ya watu wanakufuata na kukuambia uwaambie Habari za ndugu yako yule (yaani maana yake wanataka habari za kumzungumzia kutoka kwako)..Sasa hapo ili kuizuia dhambi ya umbea na usengenyaji..na dhambi ya kumwumiza mwingine kwa kutoa siri zake nje…utawaambia tu wale watu waliokuja kutafuta umbea kutoka kwamba “sifahamu mengi sana kuhusu huyo mtu labda mngeenda kumwuliza mwenyewe”…Sasa hapo umetumia Uongo kuwadanganya kwamba hujui mengi kuhusu yule mtu, ili hali unafahamu mengi..Lakini kwasababu umetumia busara kumfichia ndugu yako aibu yake..basi hujafanya dhambi na Mungu atakubariki.

Lakini ukasema kwamba mimi sio mwongo ni mkweli…na kuwaambia wale watu ndio nafahamu kila kitu wacha nianze kutiririka…japokuwa yote utakayoyasema yatakuwa ni ukweli kuhusu yule mtu lakini mbele za Mungu una dhambi.

Au umepishana na mtu mbaya anatafuta Albino, na anakuuliza hivi mtaa huu kuna mtu ambaye ni Albino nataka tufanye dili, na wewe hapo moyoni ukijua kuwa huyu ni mwalifu, na huku unaona kabisa hapo mtaani kwenu yupo mtu wa namna hiyo..na kwa busara ukamwambia yule mtu hakuna mtu wa namna hiyo mtaani kwetu..hapo utakuwa umetumia uongo lakini uongo wa busara wa kuokoa Maisha ya wengine wasio na hatia hivyo, Bwana atakubariki…lakini ukaanza kueleza kila jambo hapo umesema ukweli lakini ukweli wenye dhambi nyuma yake…Na wengi hawafahamu kuwa shetani japokuwa ni baba wa uongo lakini wakati mwingine pia anazungumza ukweli….lakini ukweli wake anaouzungumza ni ukweli unaopotosha…Kwahiyo upo uongo unaojenga na ukweli unaopotosha vile vile…(Kufahamu juu ya ukweli unaopotosha unaweza kututumia ujumbe tutakutumia somo hilo).

Kwahiyo ndio maana Mungu pia aliwabariki hawa wazalishaji wa ki-Misri kwa busara walizotumia…Ingawa walitumia uongo lakini ulikuwa ni kwa lengo la kuokoa Maisha ya Watoto wasio na hatia.

Na kuna mifano mingi katika biblia watu walitumia uongo unaojenga na Mungu akawabariki…kasome Habari za Yaeli katika Waamuzi 4:17-24, na jinsi alivyobarikiwa kuliko wanawake wote katika Waamuzi 5:24, Hali kadhalika kasome Habari za Elisha katika 2Wafalme 6:19-20, na kasome pia Habari za Rahabu yule kahaba katika Yoshua 2:3-7 n.k

Lakini hiyo haifungua fursa ya kuzungumza uongo kila mahali kwa kisingizio kwamba ni busara tunatumia…Sio unaulizwa wewe ni mkristo unajibu la! Kwa kuogopa kufa..kwa kisingizio kwamba unatumia uongo kwa busara kujiokoa Maisha yako!, hiyo siyo busara bali ni kumkana Kristo, na Biblia inasema tuwe tayari hata kuutoa uhai wetu kwa ajili yake na alisema pia anikanaye mimi nami nitamkana mbele ya Baba yangu na malaika zake siku ile. (Mathayo 10:33)…

Vivyo hivyo sio unaona mtu ni mwasherati kanisani unamfumbia macho na kusema unatumia busara kumhifadhi…watu wote wanaofanya uasherati kanisani kwa makusudi baada ya kuijua kweli na Neno la Mungu, biblia imesema waondolewe, wasifichwe..(kasome 1Wakorintho 5). Hali kadhalika na wauaji, watukanaji, waizi na walevi kanisani…

Hali kadhalika hatupaswi kuambiana uongo kwa sababu nyingine yoyote, Ndugu yako anakuuliza upo sehemu fulani wewe unamwambia sipo hapo, kwasababu tu hutaki aje..huo ni uongo wa yule adui, Unaulizwa leo umesali unasema ndio..na wakati hujasali huo ni uongo wa adui..

Bwana atusaidie tuwe na busara.

Maran atha.

Mada Nyinginezo:

UKWELI UNAOPOTOSHA.

NITAPOKEAJE NGUVU YA KUSHINDA DHAMBI?

Mahuru ndio nini?

KUMBUKA, VIVUKO VYA YORDANI VINAKUNGOJA MBELENI.

MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.

https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/maswali-na-majibu/

Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/04/23/je-mtu-anaweza-kusema-uongo-na-mungu-akambariki/