by Admin | 5 August 2020 08:46 am08
Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. Na mistari mingine mingi ya faraja ..kwa link hii >> https://chat.whatsapp.com/LO2BncRILtiAlnRYfZWG2V
Mistari ya biblia kuhusu upendo.
Upendo ndio nguzo ya kwanza katika Ukristo. Unaweza ukawa na vyote, lakini ukikosa upendo wewe mbele za Mungu si kitu kabisa,
Biblia inazungumza juu ya upendo wa aina 4:
1 Wakorintho 13:1-8
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. (1Yohana 4:8)
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.(1Petro 4:8)
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (Yohana 13:34-35)
Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. (Mithali 10:12)
Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. (1Yohana 4.11)
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.(1Wakoritho 16:14)
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.(Wakolosai 3:18-19)
Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. (Wimbo 3:4)
Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu, Nao wa kuume ungenikumbatia. (Wimbo 8:3)
Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.( Wimbo 8: 6)
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. (Marko 10:6-9)
Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.( Luka 6:27-30)
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. (Mathayo 5:43-48)
Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. (Warumi 12:20-21)
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.(Warumi 12:21)
Upendo huu ndio upendo wa hali ya juu kuliko yote (Agape), upendo wa kujitoa wakfu, usiojali hali, usiojali uzuri au ubaya wa mtu, usio na chembe yoyote ya mapungufu, Upendo wa Mungu.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16)
Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. (1Yohana 4:9-12)
Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. (1Yohana 4:19)
Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. (Yohana 15:12-13)
Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; (Kumbukumbu 7:9)
*****
Hivyo mimi na wewe ili Upendo wa namna hii uingie ndani yetu, Ni sharti kwanza tumpende yeye mwenye Upendo huo.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. (1Yohana 4:16)
Hiyo ndilo kusudi la kwanza la sisi kuwepo hapa duniani..Kumpenda Yeye.
Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Marko 12:29-30)
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/08/05/mistari-ya-biblia-kuhusu-upendo/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.