by Admin | 1 September 2020 08:46 pm09
Sala ya Baba yetu/ Sala ya Bwana.
Sala hii inapatikana katika sehemu kuu mbili kwenye biblia..
“9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
2. Na ya pili ni Luka 11:1-4
“1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu]”.
Sala hii inachukuliwa kirahisi rahisi na watu wengi, kama ni sala kutamka tu, sekunde nne,,tano umemaliza..
Lakini sivyo ambavyo Bwana Yesu alimaanisha pale.. Kumbuka wanafunzi wake walipomuuliza Bwana tufundishe jinsi ya kusali, walikuwa wanamaanisha kweli kufahamu kwa undani jinsi ya kusali, Walikuwa wanataka kujua siri ya Bwana Yesu kujibiwa maombi yake na Mungu ni nini?, walikuwa wanatamani kujua siri za kufanya maombi yao yawe na nguvu mbele za Mungu.. Walikuwa wanahitaji muongozo sahihi.
Hivyo usifiri waliambiwa watamke maneno yale tu machache ni tayari wameshasali, na sala zako zimeshasikiwa, hapana kama na wewe ulikuwa na mtazamo huo kama mimi..Basi leo ujue jinsi ya kusali mbele za Mungu kama Bwana Yesu alivyotuelekeza/
Ni kwa namna gani tusali sala ya Baba yetu/sala ya Bwana ipasavyo?
Kwa ufupi ni kuwa, maneno yale yalikuwa kama mwongozo tu, kama Ilani, kama ramani ya mtu anaposalia apite wapi na wapi,..Ili maombi ya Mtu yawe yana hoja za nguvu na mashiko, yafuate vigezo vipi na vipi.
Unapoomba sio tu, kuzungumza maneno ilimradi maneno tu, muda uende, fahamu, kanuni za uombaji, na kanuni zenyewe ndio hizo Bwana Yesu alizozihorodhesha hapo. Kipengele kimoja hadi kingine ni eneo la kuomba, kwa mfano anapoanza kwa kusema, Baba yetu uliye mbinguni..Hicho ni kipengele kimojawapo kama utangulizi wa maombi yako yafikije kwa Baba..
Sasa kwasababu somo hili tulishaliandika kwa urefu..Fungua hapa, ili uanze sasa kupitia kipengele kimoja hadi kingine, na mwisho wa somo hilo utakuwa tayari sasa umefudhu kuwa mwombaji mwenye nguvu katika ulimwengu war oho sawasawa na maagizo ya Yesu.
Fungua sasa hapa usome..>>>>>> ZIFAHAMU HOJA SABA ZENYE NGUVU MBELE ZA MUNGU.
Bwana akubariki.
Masomo Mengineyo:
RABI, UNAKAA WAPI?
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
https://wingulamashahidi.org/2019/05/13/zifahamu-huduma-kuu-10-za-shetani-duniani/
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
UNYAKUO.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/01/sala-ya-baba-yetu-sala-ya-bwana/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.