Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?

by Admin | 5 Septemba 2020 08:46 mu09

SWALI: Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi/manukato (perfumes)?


JIBU: Sio vibaya kujipaka mafuta usoni au mwilini, ili kuondoa ule mpauko wa asili, mafuta hususani yale ya asili ni mazuri kwa ngozi, lakini pia sio amri kwamba lazima tujipake mafuta, hata hivyo ngozi zetu huwa zinatoa zenyewe mafuta yake ya asili.

Lakini yapo mafuta ya kuchubua ngozi, na yenye marashi makali, hayo ni kinyume na maandiko kuyatumia kwasababu lengo lake ni kubadilisha maumbile, ambayo maudhui yake ni Udunia!..Biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na pia miili yetu sio mali yetu wenyewe, ni mali ya Mungu, hivyo hatupaswi kuibadilisha kutoka katika hali yake ya asili na kuifanya tutakavyo sisi (1Wakorintho 6:19).

Sasa unaweza kuuliza ni wapi katika agano jipya tumepewa ruhusa ya kutumia mafuta?

Mathayo 6: 16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

17  Bali wewe ufungapo, JİPAKE MAFUTA KİCHWANİ, UNAWE USO;

18  ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”

Hayo ni maneno yaliyozungumzwa na Bwana Yesu mwenyewe.

Swali lingine ni je! Ni mafuta gani yanayofaa?..Hakuna orodha maalum  ya mafuta yanayofaa, kikubwa mafuta yoyote yale yawe ya kiwandani au ya asili ambayo hayana kemikali nyingi na hayana marashi makali yanafaa kutumika.

Na Marashi ni hivyo hivyo, yapo marashi ya nguo..ambayo lengo lake ni kufanya nguo isitoe harufu aidha ya jasho au ya kitu kingine kisichofaa. Nayo pia sio vibaya kuyatumia, ilimradi tu yasiwe na maudhui ya kishetani. Marashi yanayotumika mengi siku hizi yana maudhui ya kidunia, marashi mtu anayotumia ambapo mtu aliyesimama mita 2 mbele yake au nyuma yake anasikia harufu yake, tayari lengo la marashi hayo sio kuondoa harufu bali kuvuta hisia kutoka kwa mwingine…jambo ambalo sio sawa.

Kiwango cha marashi kinapaswa kiwe kidogo sana (kiasi kwamba wewe mhusika ndio ukisikie tu, au mpaka mtu akusogelee karibu sana, ndio aweze kusikia)…

Katika biblia marashi yametafsiriwa sehemu kadha wa kadha kama “Marhamu” au “Manukato”. Unaweza kupitia mistari ifuatayo binafsi (Mathayo 26:7-13, Marko 14:3, Marko 16:1).

Lakini pia sio amri kwamba ni lazima tutumie marashi!.. Pengine ni vizuri zaidi kutoyatumia kabisa kuliko kuyatumia. Marashi yetu yanayompendeza Mungu ni Maombi yetu kwake, na utakatifu wetu.

Ufunuo 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa MANUKATO, AMBAYO Nİ MAOMBİ YA WATAKATİFU”.

2Wakorintho 2:14  “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.

15  Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;

16  katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo”

Hivyo tukiwa maridadi wa mwilini, tukanukia vizuri na huku rohoni tunatoa harufu mbaya, hatusali, hatufungi, hatuombi, hatuishi maisha ya kumpendeza yeye..basi mbele za Mungu tunapeleka harufu mbaya.

Lakini tukiwa waombaji, tukimwomba Mungu rehema, na neema..pamoja na tukiwaombea na wengine na kuliombea kanisa, na tukiishi maisha masafi, basi tutakuwa ni lulu mbele za Mungu.

Mungu atasaidie katika hilo.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KUJIPAMBA NI DHAMBI?

MSAMARIA MWEMA.

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

MIGUU ILIYO MYEPESI KUKIMBILIA MAOVU, NI CHUKIO KWA BWANA.

UWEZO WA KIPEKEE.

Rudi Nyumbani:

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/05/je-tunaruhusiwa-kujipaka-mafuta-au-kujipulizia-marashi/